Utangulizi 1Timotheo 3:1-13 Timotheo alizaliwa huko Listra akiwa na baba Myunani na mama Myahudi ... more Utangulizi 1Timotheo 3:1-13 Timotheo alizaliwa huko Listra akiwa na baba Myunani na mama Myahudi (ambaye alimfundisha Maandiko tangu utoto). Paulo alipofika Listra katika safari yake ya pili ya kitume (Mdo.16:1-3), alimchagua Timotheo ambaye alishirikiana na Paulo hadi mwisho wa huduma yake. Timotheo mwenyewe alifungwa lakini hatimaye aliachiwa huru (Ebr.13:23). Waraka wa kwanza kwa Timotheo uko katika mfumo wa mazungumzo ambayo ni ya kibinafsi sana. Paulo anamwelekeza Timotheo kuhusu sifa na wajibu wa viongozi mbalimbali katika kanisa. Pia anatoa mwongozo kwa Timotheo katika wajibu wake wa kichungaji, akimwelekeza majukumu, pamoja na yale yampasayo katika imani sahihi, mwenendo mnyofu na uadilifu. Waraka wa kwanza na wa pili kwa Timotheo na wa Tito kwa kawaida hutambuliwa kama nyaraka za Kichungaji zilizoandikwa na Paulo. Paulo aliandika waraka huu karibu na kufa kwake. Alimwandikia Timotheo msaidizi wake, ambaye alikuwa amemwacha huko Efeso kusahihisha matatizo kadhaa katika kanisa hilo. Wakati huu kulikuwa na matatizo kuhusu mafundisho ya Kikristo, mwenendo wa kanisa, uongozi wa kanisa na mambo kadha wa kadha kuhusu mwenendo uwapasao wakristo. Paulo aliandika ili kumpa Timotheo maagizo kuhusu mambo haya kusudi kanisa lifanye kazi yake vema. Aliandika pia kumtia moyo Timotheo asichoke katika maisha yake ya kikristo, bali aishi maisha ya ukamilifu kwa utukufu wa Mungu. Pia anatoa masharti maalumu kuhusu viongozi wa kanisa. Muda mfupi tu baada ya hili alikamatwa na kurudishwa tena Rumi kama mfungwa, ambako ndiko alikoandikia Waraka wa pili kwa Timotheo. Paulo anakazia kwamba wakristo inawapasa kuifahamu kweli na kuitetea dhidi ya mafundisho ya uongo yanayojitokeza. Pia hawana budi kuishi maisha yanayofanana ya mafundisho hayo ili Shetani asipate nafasi kuwateka watu wa Mungu.

Uploads
Drafts by Edward Saimon
Teaching Documents by Edward Saimon