Mazingira
Mazingira ni jumla ya mambo yote yanayomzuguka kiumbe katika maisha yake. Kwa hiyo kila unacho kiona katika maisha ni mazingira yako.
Mazingira huweza kuundwa na vitu mbalimbali; yanaweza kuwa ya asili (kama misitu, milima, maziwa, mabonde, mito, bahari n.k.) au ya kutengenezwa na binadamu (kama majengo, viwanda n.k.).
Hivyo tunapaswa tuwe makini katika kujenga mazingira yetu kwa sababu vitu vingine huyaharibu, kama vile uchafuzi wa hewa, uchafuzi wa bahari, uchafuzi wa ardhi, n.k. Tunapaswa kutunza mazingira yetu kwa sababu hali ya kilimo na ufugaji si nzuri, hivyo basi tupande miti kwa wingi, tutunze vyanzo vyetu vya maji, na kutumia maji vizuri, hasa katika shughuli za kilimo, ili kuliepuka tatizo hili, na pia kumtanguliza Mungu katika kazi zetu za kilimo na ufugaji za kila siku.
Mazingira yanaweza kuhusu:
- Hifadhi ya mazingira
- Uharibifu wa mazingira, vitu vinavyoweza kuchafua mazingira kama vile viwanda, wanyama n.k.
- Kujenga mazingira, ujenzi wa eneo ili kuwezesha shughuli za binadamu
- Biofizikia ya mazingira, pamoja na mwingiliano wa kemikali zinayoathiri viumbe hai
- Mifumo ya mazingira, maeneo ya mfumo wa kimwili ambayo yanaweza kuingiliana na mfumo wa mazingira na kubadilishana molekuli, nishati n.k.
- Sanaa ya mazingira
- Mazingira pandikizi
- Sera ya mazingira
- Saikolojia ya mazingira
- Ubora wa mazingira
- Sayansi ya mazingira, utafiti wa mwingiliano kati ya hali ya kimwili, kemikali na majumuisho ya vitu vinavyohusu mazingira ya biolojia
- Mfululizo wa mazingira, LPs, kaseti na CD zinazotoa milio ya asili
- Maarifa ya mazingira
- Mazingira ya asili, viumbe hai na visivyo hai ambavyo vimetokea kiasili duniani
- Mazingira ya kijamii, tamaduni ambazo mtu hufuata
- Ekolojia, ubora wa kibiolojia mara kwa mara huchanganywa katika mtazamo wa mazingira kwa ujumla
- Harakati za mazingira
- Uboreshaji wa mazingira, unahusiana na utunzaji wa mazingira
- Orodha ya masuala ya mazingira
- Mazingira ya mezani, graphical user interface kwa kompyuta
- Mazingira yanayobadilikabadilika, sera ya kutambulisha mchakato wa kimazingira
- Mwingiliano wa maendeleo ya mazingira, aina ya programu za kompyuta ya kusaidia katika kuendeleza wataalamu wa kompyuta ili kutengeneza programu
- Mazingira ya wakati, hali ya mashine isiyo halisi ambayo inatoa huduma ya kuprogramu michakato au mipango ya kuprogramu wakati kompyuta ikiendelea kufanya kazi
Kanuni kuhusu ulinzi wa mazingira
Nchi mbalimbali zina kanuni za ulinzi wa mazingira. Kwa mfano katika nchi za Marekani, kuna kanuni kuhusu ulinzi wa wanyama wanaokaribia kudidimia. Kanuni hii yaitwa Endangered Species Act (ESA). Pia kuna Convention on International Trade in Endangered Species of Wild Flora and Fauna (CITES). Endangered Species Act ilitengenezwa mwakani 1973 na rais Nixon alipoona kuwa kuna wanyama wanaodidimia kwa haraka sana.
Barani Afrika, ulinzi wa mazingira waendeshwa pia japo kuna matapeli wanapenda sana kukiuka sheria ili wajitajirishe kwa kuwinda wanyama kiharamu.
Tazama pia
- Category:Mazingira kwa makala zinazohusiana na athari za shughuli za binadamu katika mazingira
- All pages beginning with "Mazingira"
Viungo vya Nje
https://www.nature.org/ourinitiatives/regions/africa/index.htm