Abdi Kassim
Abdi Kassim Sadalla (alizaliwa Zanzibar 19 Oktoba 1984) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka Tanzania. Mwaka 2004 alianza kucheza timu ya Mlandege / Zanzibar baadae akahamia Mtibwa Sugar F.C. Hadi mwaka 2013 alihamahama klabu za Tanzania Bara kama vile Young Africans S.C. na Azam F.C. akiwa pia katika timu ya taifa.
Abdi Kassim Sadalla | ||
Maelezo binafsi | ||
---|---|---|
Tarehe ya kuzaliwa | 19 Oktoba1984 | |
Mahala pa kuzaliwa | Zanzibar, Tanzania | |
Urefu | 1.86 m | |
Nafasi anayochezea | kati | |
Klabu za ukubwani | ||
Miaka | Klabu | |
Mlandege, Mtibwa Sugar, Young Africans, Azam FC , UiTM FC | ||
Timu ya taifa | ||
Tanzania | ||
* Magoli alioshinda |
Miaka 2014 - 2016 alichezea UiTM F.C. kutokea nchini Malaysia. [1]. Baada ya kurudi aliingia kwa Jang'ombe Boys[2].
Kazi ya kimataifa
haririWakati mwingine aliitwa BABI au pia Ballack wa Unguja. Kassim alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao katika uwanja mpya wa Tanzania jijini Dar es Salaam, Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa, kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Uganda.
Kassim alijulikana kwa uwezo wake wa kulenga mbali. Anapendelea mguu wake wa kushoto.
Marejeo
hariri- ↑ Abdi Kassim, tovuti ya transfermarkt.com, iliangaliwa Desemba 2019
- ↑ Abdi Kassim Sadalla, tovuti ya National Football Teams
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Abdi Kassim kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |