Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                

Hagia Sophia ni jina la Kigiriki (Ἅγια Σοφία, yaani "Hekima takatifu"; kwa Kituruki Ayasofya) la kanisa kubwa mjini Istanbul - Konstantinopoli lililobadilishwa kuwa msikiti tangu mwaka 1453 isipokuwa lilipofanywa makumbusho miaka 1934-2020.

Hagia Sophia mjini Istanbul
Hagia Sophia kwa ndani
Mozaiki ya Yesu katika ukuta wa Hagia Sophia

Historia

hariri

Ujenzi wa kanisa hilo ulianza mwaka 532 kwa amri ya Kaisari Justiniani I mtawala wa Roma ya Mashariki au Ufalme wa Byzanti. Alitaka kuwa na kanisa kubwa kuliko yote duniani akafaulu kwa sababu Hagia Sofia ilikuwa ukumbi mkubwa duniani hadi mwaka 1520. Jengo lilikamilishwa baada ya miaka mitano na Justiniani alipoingia mara ya kwanza aliita, "Suleimani, nimekushinda", akimfikiria mfalme Suleimani wa Israeli ya Kale aliyejenga hekalu la Yerusalemu.

Mwaka 1453 Waturuki Waislamu waliteka mji wa Konstantinopoli na kuufanya mji mkuu wa Dola la Osmani. Hapo Hagia Sofia likabadilishwa kuwa msikiti na Waturuki wakatamka jina la kigiriki kama "Ayasofya". Jengo la kanisa likaongezewa minara minne ya mtindo wa Kiislamu.

Baada ya anguko la Waosmani katika vita kuu ya kwanza ya dunia kiongozi wa taifa Kemal Atatürk akaamuru jengo liwe makumbusho, lakini tarehe 24 Julai 2020 limeanza kutumika tena kama msikiti.

Viungo vya Nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.