Hathor
Hathor alikuwa mmoja wa miungu katika dini ya Misri ya Kale. Alikuwa mungu wa kike aliyepewa nafasi mbalimbali katika imani ya watu. Wakati wa nasaba ya kwanza aliabudiwa kwa umbo la ng'ombe. Baadaye aliaminiwa kuhusika na anga akaabudiwa kama mama wa miungu mingine, hasa mungu Ra aliyekuwa Jua. Alikusika pia na mapenzi, amani, uzuri, sanaa na muziki.
Mwonekano
haririHathor alioneshwa katika maumbo manne tofauti. Kwa sura ya kibinadamu, Hathor alikuwa na kichwa cha ng'ombe na pembe mbili za ng'ombe, kwa sababu ng'ombe walikuwa wanyama wenye thamani kubwa.
Katika moja ya maumbo yake ya kinyama, alikuwa ng'ombe mwenye ankh. Ankh ilikuwa ishara ya uhai.
Umbo lingine la kinyama la Hathor lilikuwa simba mkali.
Ishara ya Hathor ilikuwa ng'ombe anayebeba duara ya Jua kati ya pembe zake. Wamisri waliwaza kwamba Hathor anamzaa Ra, mungu wa Jua, kila asubuhi akiendelea kumbeba angani kati ya pembe zake.
Marejeo
hariri- John Coleman Darnell:Hathor Returns to Medamud, Studien zur altägyptischen Kultur 22 (1995): 47-94
- Robin Gillam:Priestesses of Hathor: Their Function, Decline and Disappearance, 1995, Journal of the American Research Center in Egypt
- Carolyn Graves Brown, Dancing for Hathor-women in ancient Egypt, Continuum. ISBN 978-1847250544
- Lesko, Barbara S.: The great goddesses of Egypt, University of Oklahoma Press. ISBN 978-0806132020, kupitia archive.org
- Hathor Article by Caroline Seawright Archived 2010-05-13 at the Wayback Machine
- Domain of Het-Hert (Hathor) Archived 2019-01-14 at the Wayback Machine