Hema
Hema ni kibanda chepesi kinachofanywa na kiunzi cha ndani na ganda la nje la kitambaa, plastiki au ngozi. Kazi yake ni kukinga dhidi ya jua, mvua, baridi au athari nyingine za hali ya hewa. Hema ni rahisi kufumuliwa na kupelekwa mahali pengine kwa matumizi mapya.
Katika jamii zinazofuata maisha ya uhamaji hema ni kawaida badala ya nyumba imara, kwa mfano wafugaji wanaohamahama pamoja na kondoo, mbuzi, ng'ombe au ngamia zao.
Mahema madogo yanatumiwa pia kama kinga ya muda kwa burudani kama camping au matembezi marefu. Mahema makubwa zaidi hutumiwa na jeshi kwa kambi za muda, pia wakati wa maafa kama watu hawana nyumba tena: kwa mfano baada ya tetemeko la ardhi au mafuriko. Mahema makubwa sana zatumiwa kwa mikutano mahali pasipo ukumbi mkubwa kiasi cha kutosha.
Katika ukulima wa kisasa hema pia hutumika kukuzia mimea kama vile katika ukuzaji wa mimea bila mchanga unaojulikana kwa Kiingereza kama Hydroponic. Mahema hayo maarufu kama Grow Tents yana miundo na ukubwa tofauti na hukinga mimea kutokana na athari za hali ya anga, wadudu na wanyama waharibifu au kukuziwa mimea inayohitaji kutunzwa kwa makini[1]. Hema za kukuzia mimea ni maarufu sana na wakulima wa miche na wakulima wa mbangi.
Picha
hariri-
Mahema ya kijeshi wakati wa Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani, 1865
Tanbihi
hariri- ↑ "7 Reasons to Use a Grow Tent". The Home Depot Garden Club (kwa American English). 2017-12-12. Iliwekwa mnamo 2019-07-02.
Marejeo
haririViungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hema kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |