Majira ya joto
Majira ya joto (pia: chaka; kwa Kiingereza Summer) ni mojawapo kati ya majira manne ya kanda za wastani, na halijoto yake ni ya joto kuliko majira mengine.
Inaweza kulinganishwa na chaka ambayo ni kipindi cha joto katika Afrika ya Mashariki.
Kadiri ya umbali na ikweta, mchana ni mrefu na usiku ni mfupi. Ndiyo sababu majira hayo yanaitwa ya joto.
Sehemu nyingine joto ni kali kiasi kwamba kwa miezi 2-3 shule huwa zimefungwa.
Yanafuata majira ya kuchipua (kwa Kiingereza "Spring") na kutangulia majira ya kupuputika majani (kwa Kiingereza "Fall" au "Autumn").
Majira hayo yanatokea duniani kwa nyakati tofauti kadiri eneo husika lilivyo kaskazini au kusini kwa ikweta. Hata katika nchi ileile, kwa mfano Kenya, majira ni tofauti upande huu na upande huu wa ikweta.
Tanbihi
haririViungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Majira ya joto kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |