Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                

Mapokeo (kutoka kitenzi kupokea) ni imani au desturi zilizorithishwa katika kundi au jamii fulani zikiwa na maana maalumu tangu zamani.[1]

Maadhimisho ya sikukuu yanaweza kuendelea kama mapokeo, kwa mfano katika meza na mapambo haya ya Krismasi huko Polandi.

Kati yake kuna sikukuu, salamu na mavazi ambayo hayafai sana kutumika lakini yana maana kijamii, hasa kwa kumtambulisha mtu aliyeyavaa (k.mf. askari, mwanasheria, mtawa).

Mapokeo yanaweza kudumu na kubadilika kwa miaka elfuelfu, lakini yanaweza kuanzishwa na kuenea haraka.

Jina la Kiingereza "tradition" linatokana na kitenzi cha Kilatini tradere, yaani kueneza au kukabidhi.

Wazo hilo linatumika pia katika siasa, falsafa na dini, k.mf. kwa kwenda kinyume cha usasa.

Katika Ukristo

hariri

Katika Ukristo, kuna mapokeo ya Kanisa yanayozingatiwa sana na baadhi ya madhehebu (hasa Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki, lakini pia Waanglikana na wengineo) kwa sababu asili yao ni wakati wa Mitume wa Yesu, ambao ulikuwa bado wakati wa Ufunuo wa Mungu katika imani ya madhehebu hayo.

Mapokeo ya namna hiyo yanaitwa mapokeo ya Mitume kwa kuyatofautisha na mapokeo mengi yaliyotokea baadaye na ambayo yanaweza kuwa mazuri lakini pia mabayaː kwa vyovyote hayambani Mkristo kwa msingi wa imani.

Hata hivyo madhehebu mengine, hasa ya Uprotestanti, yanakataa yale yote yasiyopatikana wazi katika Biblia ya Kikristo.

Tanbihi

hariri
  1. Thomas A. Green (1997). Folklore: an encyclopedia of beliefs, customs, tales, music, and art. ABC-CLIO. ku. 800–. ISBN 978-0-87436-986-1. Iliwekwa mnamo 5 Februari 2011.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)