Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nzi
Nzi-nyumbani (Musca domestica)
Nzi-nyumbani (Musca domestica)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Diptera (Wadudu wenye mabawa mawili tu)
Nusuoda: Brachycera (Diptera wenye vipapasio vifupi)
Zetterstedt, 1842
Ngazi za chini

Oda za chini 6:

Nzi ni wadudu wadogo wa nusuoda Brachycera katika oda Diptera (yaani “wenye mabawa mawili”). Kwa asili jina hili limetumika kwa wadudu wa familia Muscidae, lakini kwa sababu spishi nyingi za Brachycera hazina majina ya Kiswahili, “nzi” linapendekezwa kama jina kwa Brachycera wote. Nusuoda nyingine ya Diptera, Nematocera, inashirikisha mbu na jamaa wao.

Diptera wote wana mabawa mawili tu yaliyopo kwa mesotoraksi. Mabawa ya nyuma ya asili yamepunguzika na kubadilika kuwa virungu (halteres) ambavyo vinasaidia mdudu ajue mkao wake na mabadiliko ya mwelekeo (kama aina ya gurudumu tuzi). Vipapasio vya Brachycera ni vifupi na vina mapingili machache kuliko Nematocera, mara nyingi matatu tu lakini hadi 7. Spishi nyingi zinabeba unywele (arista) juu ya pingili la tatu la vipapasio. Nzi hawana sehemu za kinywa zinazoweza kutumika kwa kutafuna, kwa hivyo hula chakula cha majimaji au cha chembe ndogo (kama chavua).

Lava wa nzi hawana miguu na wanafanana na minyoo. Kwa kawaida wana meno mawili yaliyopindika (kama kulabu) na spirakulo mbili kwenye nyuma ya kiwiliwili. Huonekana mara nyingi katika nyama iliyooza na katika matunda.

Spishi kadhaa za Afrika

hariri
  Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nzi kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.