Kiroboto
(Elekezwa kutoka Viroboto)
Kiroboto | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Jike la kiroboto wa binadamu (Pulex irritans)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Nusuoda 4: |
Viroboto ni wadudu wadogo (mm 1.8-3.3) wa oda Siphonaptera. Sehemu za kinywa zimeungana katika kimrija kitumikacho kudunga ngozi na kufyonza damu.
Wadudu hao hawana mabawa, lakini wanaweza kuruka mbali sana ikilinganishwa na ukubwa wao. Kiroboto wa binadamu anaweza kuruka juu sm 18 na mbele sm 33 (sawa na m 90 ikiwa mtu wa m 1.8 angaliweza kuruka kama kiroboto).
Viroboto wanaweza kurithisha magonjwa, k.m. tauni (hurithishwa na Kiroboto wa Panya).
Spishi zinazojulikana sana
hariri- Ctenocephalides canis, Kiroboto wa Mbwa (Dog flea)
- Ctenocephalides felis, Kiroboto wa Paka (Cat flea)
- Pulex irritans, Kiroboto wa Binadamu (Human flea)
- Xenopsylla cheopis, Kiroboto wa Panya (Tropical rat flea)
Picha
hariri-
Jike la kiroboto wa kuku (Ceratophyllomorpha)
-
Jike la kiroboto wa mbwa (Pulicomorpha)
-
Jike la kiroboto wa paka (Pulicomorpha)
-
Jike la kiroboto wa panya (Pulicomorpha)
Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kiroboto kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |