Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Plataia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
The printable version is no longer supported and may have rendering errors. Please update your browser bookmarks and please use the default browser print function instead.
Mabaki ya ukuta wa Plataia ya Kale

Plataia au Plataea (kwa Kigiriki Πλάταια) ulikuwa mji wa Ugiriki ya Kale, ulioko Ugiriki kusini, takriban kilomita 60 upande wa magharibi mwa Athens, kusini mwa Thebes.

Plataia ilikuwa mji rafiki wa Athens na katika vita dhidi ya Waajemi jeshi la Plataia lilipigana pamoja na Waathens kama kwenye mapigano ya Marathon mnamo mwaka 490 KK. Mapigano ya Plataia yaliyotokea mnamo 479 KK karibu na mji yaliyeta ushindi wa mwisho wa Wagiriki dhidi ya Uajemi.

Plataia iliharibiwa katika Vita ya Peloponnesi na Thebes na Sparta mnamo 427 KK ikajengwa upya mnamo 386 KK na kubomolewa tena 373 KK.

Mji wa kisasa wa Plataies umejengwa karibu na magofu yake.

Kilima cha mazishi cha Waplataia waliouawa kwenye Mapigano ya Marathoni

Marejeo

Viungo vya nje