Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Shirika Lisilo la Kiserikali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Asasi isiyo ya kiserikali)
mkutano wa asasi zisizo za kiserikali duniani mwaka 2019

Shirika Lisilo la Kiserikali (mara nyingi kwa kifupi cha Kiingereza kama "NGO" kwa "non-governmental organization") ni maungano ya watu wanaoshirikiana pamoja kwa kulenga shughuli za jamii kwa jumla. Haipokei maagizo kutoka kwa serikali wala hailengi faida ya kifedha kwa watu wanaoendesha shirika.

Mashirika yasiyo ya Kiserikali yako kwenye ngazi ya miji, maeneo, kitaifa na kimataifa.

Kati ya shirika zisizo za serikali zinazojulikana zaidi kimataifa ni Msalaba Mwekundu, makanisa na vyama vyao kama vile Caritas au Diakonia, shirikia nyingine za kidini zinazotoa huduma za umma, Amnesty International, Madaktari wasio na Mipaka-MSF, Oxfam na wengi wengine. Jumla la shirika zisizo za serikali zinazofanya kazi kwenye kiwango cha kimataifa hukadiriwa na Umoja wa Mataifa kufikia takriban 40,000. Umoja wa Mataifa hujaribu kuzikusanya kwenye mikutano za kijamii za dunia.

Shirika hizi zapata pesa zao kwa njia ya zawadi na michango kutoka kwa watu ama wanachama au umma kwa jumla. Mara nyingi zinatumia pia pesa kutoka serikali mbalimbali kwa sababu zina nafasi ya kufikia mahali ambako serikali haziwezi kutuma watumihsa kwa sababu za kisiasa.

Kwa mfano shirika zisizo za serikali zilifanya kazi ya kutunza wakimbizi katika Sudan ya kusini wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe zikitumia pesa za Umoja wa Ulaya au serikali mbalimbali zilizotengwa kwa usaidizi wa watu matatizoni. Lakini kutokana na sababu za kisiasa serikali hizi hazikuweza kupeleka usaidizi kwa watu wenyewe pale walipokaa katika shida ila shirika zisizo za serikali zilikuwa na uhuru wa kujadiliana na pande zote na kuingia kila mahali ikiwezekana.

Tazama pia