Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Ice-T

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ice-T
Ice-T, Machi 2011
Ice-T, Machi 2011
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Tracy Marrow
Amezaliwa 16 Februari 1958 (1958-02-16) (umri 66)
Newark, New Jersey
Asili yake Los Angeles, California, Marekani
Aina ya muziki Hip hop, heavy metal
Kazi yake Mwigizaji
Emcee
Mwanamuziki
Mtunzi wa nyimbo
Miaka ya kazi 1982 - hadi sasa
Studio Sire, Rhyme Syndicate, Priority, Atomic Pop, Melee
Ame/Wameshirikiana na Body Count
Tovuti www.IceT.com

Tracy Marrow (amezaliwa tar. 16 Februari, 1958), anafahamika zaidi kwa jina la kisanii kama Ice-T, ni rapa na mwigizaji kutoka nchini Marekani. Alizaliwa mjini Newark, New Jersey na kisha baadaye akahamia mjini Los Angeles, California. Baada ya kuhitimu masomo ya elimu ya juu, alimtukia katika Jeshi la Ulinzi la Marekani kwa takriban miaka minne. Alianza kazi ya kurap mwanzoni mwa miaka ya 1980 na aliingia mkataba na Sire Records mnamo 1987, pale alipotoa albamu yake ya kwanza, Rhyme Pays. Mwaka uliofuata, akaanzisha studio ya kurekodia iliyoitwa Rhyme Syndicate na kuweza kutoa albamu nyingine iliyokwenda kwa jina la Power. Amekuwa mwimbaji kiongozi kwenye bendi ya muziki wa heavy metal, Body Count, ambao aliitambulisha kwenye albamu yake ya mwaka wa 1991 O.G.: Original Gangster. Body Count wakatoa albamu ya kwanza iliyoitwa jina lao wenyewe mnamo mwaka wa 1992. Ice-T akawa gumzo la matata kwa kibao chake cha "Cop Killer", ambacho kilionekana kuchochea mauaji ya maafisa wa polisi. Kwa sababu ya hili, akaondoka Warner Bros. Records mnamo 1993 na badala yake katoa albamu yake ya Home Invasion kupitia studio ya Priority Records. Albamu ya pili ya Body Count ilitolewa mnamo 1994, na Ice-T akatoa albamu mbili zaidi mwishoni mwa miaka ya 1990.

Kama mwigizaji, Ice-T alianza kushiriki kwenye nyusika ndogo-ndogo katikati mwa miaka ya 1980. Mnamo 1991, Ice-T alianza rasmi shughuli za uigizaji kama mwigizaji kwenye filamu ya New Jack City. Ice-T ameonekana kwenye filamu kama vile Who's the Man? (1993), CB4 (1993), Tank Girl (1995), na Johnny Mnemonic (1995). Amecheza kama askari kanzu Odafin "Fin" Tutuola kwenye igizo la kipolisi la NBC, Law & Order: Special Victims Unit tangu 2000. Mnamo 2006, Ice-T albamu yake ya kwanza baada ya kimya cha miaka saba, Gangsta Rap.

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]
Makala kuu: Ice-T discography

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]