Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Wakapuchini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka O.F.M.Cap.)

Wakapuchini ni watawa Wafransisko wa Kanisa Katoliki.

Idadi yao inapita ndugu wanaume 10,000 duniani kote wakiongozwa na ndugu Mauro Jöhri wa kanda ya Uswisi. Ni shirika la kiume la nne kwa wingi wa watawa duniani.

Maana ya jina

[hariri | hariri chanzo]

Jina linatokana na neno la Kiitalia "cappuccio", lenye maana ya kikofia kilichoshonwa kwenye kanzu yao ya rangi ya kahawia.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Tawi hilo lilianzishwa na Mathayo wa Bascio pamoja na Ludoviko wa Fossombrone na Rafaeli wa Fossombrone mwaka 1525, ambao walilenga maisha ya kifukara kuliko yaliyofuatwa na Ndugu Wadogo wenzao.

Urekebisho huo, uliojitahidi sana kufuata kikamilifu kanuni ya Ndugu Wadogo na mifano ya mwanzilishi, Fransisko wa Asizi, ulipata kibali cha Papa Klementi VII mwaka 1528.

Baada ya hapo kutoka mkoa wa Marche shirika likaenea na kuzaa matunda mengi ya utakatifu kuanzia bradha Felix wa Cantalice hadi padri Pio wa Pietrelcina.

Mnamo tarehe 31 Desemba 2011, Wakapuchini duniani walikuwa 10.364, kati yao mapadri 6.968. Wako katika nchi 106: Afrika 1321; Amerika ya Kilatini 1720; Amerika ya Kaskazini 662; Asia-Oceania 2283; Ulaya 4378.[1]

  1. Analecta Ordinis Fratrum Minorum Capuccinorum, Roma

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  • Ordo Fratrum Minorum Capuccinorum, tovuti rasmi ya shirika
  • Capuchins in Canada - Mary, Mother of the Good Shepherd Province, official website
  • Capuchins of Ireland - Province of St. Patrick and St. Francis Ilihifadhiwa 18 Septemba 2015 kwenye Wayback Machine., official website
  • Capuchin Franciscan Order - Our Lady of Angels Province Ilihifadhiwa 1 Juni 2018 kwenye Wayback Machine., official website of Capuchin Franciscan Order in Western America
  • The Capuchin-Franciscan Province of St. Joseph (Mid-West USA), official website
  • Province of St. Joseph, official website
  • The Capuchin-Franciscans of the Province of Saint Augustine, official website
  • "Capuchin Friars Minor". Catholic Encyclopedia.
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wakapuchini kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.