Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                

Amani ya Westfalia

Amani ya Westfalia ilikuwa mapatano yaliyofanyika mwaka 1648 ili kumaliza vita ya miaka 30 katika Ujerumani na nchi za jirani. Mapatano yalimalizika katika mikutano kwenye miji ya Münster na Osnabrück.

Ulaya baada ya Amani ya Westfalia 1648;
mstari mwekundu: Mipaka ya Dola Takatifu.

Washiriki katika mapatano hayo walikuwa Kaisari Ferdinand III wa Dola Takatifu la Kiroma, watawala wengine wa madola ndani ya Ujerumani, halafu Hispania, Ufaransa, Uswidi na Uholanzi.

Kati ya matokeo ya kudumu yalikuwa uhuru wa Uswisi na Uholanzi zilizohesabiwa awali kama sehemu za Dola Takatifu, mapatano kuhusu uvumilivu kati ya Wakatoliki, Walutheri na Wareformed kama madhehebu makubwa ya Kikristo katika Ujerumani na kupungukiwa kwa madaraka ya Kaisari lakini kuongezeka kwa haki za madola madogo ndani ya Ujerumani.

Mataifa ya nje kama Uswidi na Hispania yalikuwa sasa na maeneo ndani ya Dola Takatifu na Ujerumani yenyewe; madola ya Ujerumani kama Habsburg-Austria na Brandenburg-Prussia yalitawala pia maeneo nje ya Dola Takatifu.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Amani ya Westfalia kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.