Ardabil
Ardabil (pia Ardabīl na Ardebīl , Kiajemi na Kiazeri : اردبیل) ni mji wa kihistoria kaskazini-magharibi mwa Iran. Jina Ardabil linatokana na jina la Kiajemi cha kale "Artawila", likimaanisha mahali patakatifu. [1] Ardabil ni makao makuu wa Mkoa wa Ardabil . Katika sensa ya 2011, idadi ya wakazi ilikuwa 564,365 katika familia 156,324, Wakazi wengi ni Waazeri. [2] [3] Ardabil pia inajulikana kwa patakatifu na kaburi la Safî ad-Dîn na jina lake lilikuwa chanzo cha nasaba ya wafalme wa Safavi .
Marejeo
hariri- ↑ Iranian Provinces: Ardabil
- ↑ "Ardabil". Looklex Encyclopaedia. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-09-28. Iliwekwa mnamo 2013-08-13.
- ↑ "Ardabīl". Encyclopædia Britannica. Iliwekwa mnamo 2013-08-13.
Tovuti za Nje
hariri- Vivutio vya Watalii vya Ardabil Archived 28 Machi 2010 at the Wayback Machine.
- http://www.irantour.org/Iran/province/ardabil.html Archived 7 Juni 2008 at the Wayback Machine. .
- http://www.travel-images.com/az-ardebil.html