Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                

Google ni tovuti kwenye mtandao inayotumika kutafuta kurasa na habari za kila aina. Inatumia programu inayoitwa "mashine ya kutafuta" (search engine). Jina Google limetokana na neno Googol linalomaanisha tarakimu 1 inayofuatwa na sifuri 100.

Google
Aina ya shirikaPublic
AlamaKigezo:NASDAQ
Kigezo:NASDAQ
NASDAQ-100 Component
S&P 500 Component
Tarehe ya kwanzaMenlo Park, California
(Septemba 4, 1998 (1998-09-04))[1][2]
MwanzilishiSergey Brin, Larry Page
Pahali pa makao makuu, Mountain View, California, U.S.[3]
Pahali pa watejaWorldwide
Watu muhimu
Sekta ya viwandaInternet
Computer software
Telecoms equipment
BidhaaSee list of Google products
Mapatoincrease US$ 59.82 billion (2013)[4]
Mapato kasoro ushuruincrease US$ 13.96 billion (2013)[4]
Faidaincrease US$ 12.92 billion (2013)[4]
Jumla ya maliincrease US$ 110.92 billion (2013)[4]
Thamaniincrease US$ 87.30 billion (2013)[4]
Wafanyakazi49,829 (Q1 2014)[5]
Tovutigoogle.com

Imepata mafanikio makubwa kati ya tovuti za aina hii, na kila siku takriban watu milioni 200,000 wanaitumia.[6]

Tovuti ni mali ya kampuni Google Inc. ya Marekani, lakini kampuni mama ni Alphabet Inc.. Kampuni ilianzishwa na Larry Page and Sergey Brin mwaka 1998, wakati walipokuwa wanafunzi wa chuo kikuu.

Matumizi ya Google ni bure, lakini kampuni ina mapato makubwa kutokana na matangazo ya biashara kwenye kurasa zake na thamani ya kampuni imekadiriwa kuwa bilioni za dolar 130 hivi.[7] Umaarufu wa mashine ya kutafuta ya Google umetokana na sababu mbalimbali ikiwemo kanuni zinazotumika kuzipa ukurasa daraja la mtandaoni kwa kutumia mfumo uliopewa jina la PageRank kutokana na jina la mmoja wa waanzilishi wa Google, Larry Page.[8] watangazaji wengi hujitahidi kutumia mbinu mbalimbali ili kuwa na daraja la juu kwenye mashine yake ya kutafuta.

Kiasili Google ilitengenezwa kwa kutafuta maneno kwenye tovuti na hadi leo hii matumizi yake ni makubwa. Lakini Google imeendelea kuongeza huduma nyingine kama kutafuta picha (Google Images), kutafuta mahali kwenye ramani ya dunia (Google Maps), kutafuta habari kwenye wavuti ya magazeti (Google News), video (YouTube) na mengine mengi.

Nje ya huduma za kutafuta, google imeanzisha pia huduma nyingine kama 'Google Mail' (huduma ya barua pepe) au huduma za kutunza kalenda (Google Calendar) na maandishi ya binafsi ya akaunti kwenye seva za google.

Huduma nyingine ni ile ya kutafsiri (Google Translate) yenye nafasi ya kupakia matini kutoka moja ya lugha 60 na programu inajaribu kuitafsiri kwa lugha nyingine. Kati ya lugha kubwa kama Kiingereza, Kihispania au Kifaransa matokeo ni mazuri kiasi, lakini lugha ndogo kama Kiswahili bado hayajaridhisha ingawa inaendelea kuboreka polepole.

Kuna pia jaribio la kutoa google kwa lugha ya Kiswahili lakini hii inaleta tu ukurasa wa kuingia katika tovuti iliyotafsiriwa kisehemu.

Historia

Google ni kampuni ya teknolojia iliyoundwa mnamo Septemba 1998 na Larry Page na Sergey Brin wakati walipokuwa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Stanford jijini California, Marekani. Wawili hao waliunda Google kama injini ya utaftaji wa wavuti ili kuboresha ufanisi wa kutafuta na kupata habari mtandaoni.

Jina "Google" linatokana na neno "googol," ambalo ni namba yenye 1 followed na sifuri 100. Lengo lilikuwa kuonyesha wingi wa habari ambayo injini yao ya utaftaji ilikuwa inaweza kuipata.

Google ilipata umaarufu haraka kutokana na ufanisi wake wa utaftaji na kutoa matokeo sahihi zaidi kuliko injini zingine za utaftaji wakati huo. Baadaye, kampuni hiyo iliongeza huduma zingine kama vile Gmail (barua pepe), Google Maps (ramani mtandaoni), YouTube (plartform ya video), na Android (mfumo wa uendeshaji wa simu za mkononi).

Mnamo mwaka 2004, Google iliendelea kuwa kampuni ya umma kupitia mauzo ya hisa kwenye soko la hisa la NASDAQ. Leo, Google ni sehemu ya kampuni kubwa ya teknolojia inayoitwa Alphabet Inc., ambayo ni kundi la makampuni mbalimbali yanayoshughulika na teknolojia, ikiwa ni pamoja na Google.

Google imeendelea kukua na kuwa mojawapo ya kampuni kubwa na yenye ushawishi mkubwa katika tasnia ya teknolojia, ikitoa huduma mbalimbali mtandaoni na nje ya mtandao.


Marejeo

  1. "Company". Google. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-11-17. Iliwekwa mnamo Agosti 31, 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Claburn, Thomas. "Google Founded By Sergey Brin, Larry Page... And Hubert Chang?!?". InformationWeek. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-01-07. Iliwekwa mnamo Agosti 31, 2011.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Locations - Google Jobs". Google.com. Iliwekwa mnamo 2013-09-27.
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 4.4 "Google Inc, Form 10-K, Annual Report, Filing Date Jan 29, 2013". secdatabase.com. Iliwekwa mnamo Machi 8, 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Google's Income Statement Information". Google.
  6. "Taarifa ya searchenginewatch Aprili 2011". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-04-17. Iliwekwa mnamo 2011-04-19.
  7. "taarifa ya kampuni ya Millwardbrown ya mwaka 2010". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-05-04. Iliwekwa mnamo 2011-04-19.
  8. "Google Press Center: Fun Facts". www.google.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2001-07-15.

Viungo vya nje

  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.