Liturujia ya Ugiriki
Liturujia ya Ugiriki, iliyoenea kutoka Konstantinopoli, sasa Istanbul (nchini Uturuki) ni liturujia ambayo lugha yake asili ni Kigiriki, lakini siku hizi inaadhimishwa katika lugha nyingine nyingi kukiwa na tofauti ndogondogo duniani kote.
Wanaoitumia hasa ni Waorthodoksi wote na baadhi ya Makanisa Katoliki ya Mashariki: hivyo ni ya pili kwa uenezi baada ya liturujia ya Roma.
Vitabu vyake vinaongoza Liturujia ya Kimungu (Ekaristi), Vipindi vya sala rasmi, Mafumbo matakatifu (Sakramenti) na sala, baraka na mazinguo mbalimbali, vilivyostawi katika Kanisa la Konstantinopoli.
Liturujia hiyo inahusika pia na namna maalumu za usanifu majengo, picha takatifu, muziki wa liturujia, mavazi na mapokeo zilizostawi vilevile karne hata karne kila ilikotumika.
Kwa kawaida mkusanyiko wa waamini huwa wamesimama muda wote wa ibada, na ukuta wa picha takatifu unaoitwa iconostasis unawatenganisha na patakatifu anapohudumia askofu au padri akisaidiwa na shemasi.
Ushiriki wa walei unajitokeza katika kusujudu mara nyingi na kuitikia sala na nyimbo.
Katika liturujia hiyo Biblia inatumika sana katika masomo na katika matini mengine vilevile.
Taratibu za saumu ni kali kuliko zile za Ukristo wa Magharibi na zinafuatwa katika vipindi vinne kwa mwaka: Kwaresima Kuu, Kwaresima ya Noeli, Mfungo wa Mitume na Mfungo wa Kulala kwa Bikira Maria. Pamoja na hayo, Jumatano na Ijumaa nyingi ni za kufunga chakula. Monasteri nyingi zina mfungo hata Jumatatu zote.
Historia
haririLiturujia hiyo ilianza kwa kufuata liturujia ya Siria, kwa kuwa kabla ya mwaka 381 Mashariki ya Kati ilikuwa chini ya Kanisa la Antiokia).
Mwaka huo Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli ulifanya mji huo kuwa na Patriarki wake, wa pili baada ya askofu wa Roma tu[1]. Hapo liturujia hiyo ilizidi kupata sura ya pekee kwa kuathiriwa hata za desturi za ikulu ya kaisari iliyokuwepo Konstantinopoli.
Tanbihi
haririMarejeo
hariri- Robert F. Taft, The Byzantine Rite. A Short History. Liturgical Press, Collegeville 1992, ISBN 0-8146-2163-5
- Hugh Wybrew, The Orthodox Liturgy. The Development of the Eucharistic Liturgy in the Byzantine Rite, SPCK, London 1989, ISBN 0-281-04416-3
- Hans-Joachim Schulz, Die byzantinische Liturgie : Glaubenszeugnis und Symbolgestalt, 3., völlig überarb. und aktualisierte Aufl. Paulinus, Trier 2000, ISBN 3-7902-1405-1
- Robert A. Taft, A History of the Liturgy of St John Chrysostom, Pontificio Istituto Orientale, Roma 1978-2008 (6 volumes).
Viungo vya nje
hariri- Study Text of the Divine Liturgy of Saint John Chrysostom
- Study Text of the Divine Liturgy of Saint Basil the Great
- The Divine Music Project Archived 19 Agosti 2006 at the Wayback Machine. Thousands of pages of Byzantine music in English for Byzantine rite services
- Fr. Ronald Roberson's book The Eastern Christian Churches – A Brief Survey Archived 29 Oktoba 2006 at the Wayback Machine. is the most up-to-date primer on these churches, available on-line at Catholic Near-East Welfare Association (CNEWA).
- "The Rite of Constantinople". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913. http://www.newadvent.org/cathen/04312d.htm.
- Rites of the Catholic Church Giga-catholic Website
- Byzantine rite in Italy The tradition of the Italo-Greek-Albanian Church
- The Byzantine-Slavic Rite
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Liturujia ya Ugiriki kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |