Opera
Opera ni igizo inayoimbwa katika utamaduni wa Ulaya. Waigizaji hawasemi bali huimba maneno yao. Igizo ya opera hufanywa mara nyingi katika nyumba za pekee. Pamoja na waigizaji na waimbaji kuna bendi maalumu.
Maigizo ya Opera hufuata maelezo ya kimaandishi na kila neno la mwigizaji limeandikwa. Vilevile uimbaji pamoja na muziki yote ni ya kuandikwa.
Watungaji mashuhuri wa muziki walitunga opera kama vile
- Ludwig van Beethoven
- Hector Berlioz
- Georg Friederich Händel
- Wolfgang Amadeus Mozart
- Giacomo Puccini
- Bedřich Smetana
- Pyotr Ilyich Tchaikovsky
- Giuseppe Verdi
- Richard Wagner .
Wikimedia Commons ina media kuhusu: