Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Ajali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 15:01, 29 Desemba 2009 na Muddyb (majadiliano | michango) (Sahihisho dogo tu...)
Kitalu cha benchi chaanguka katika mchezo wa soka katika chuo, kikiwabwaga mashabiki kwenye pande.

Ajali ni tukio maalumu linalotambulika na lisilotarajiwa, geni na lisilotakikana ambalo hutokea katika muda na mahali fulani bila sababu au makusudi dhahiri, lakini husababisha madhara yaliyo wazi. Ajali hudokeza kwa ujumla matokeo mabaya ambayo labda yangeweza kuepukwa au kukingwa ikiwa matukio yaliyosababisha ajali hiyo yangetambuliwa, na kurekebishwa, kabla ya tukio hilo.


Wataalam katika nyanja ya kuepuka majeraha hawatumii neno 'ajali' kuelezea matukio ambayo husababisha majeraha katika jaribio la kubainisha asili ya majeraha mengi ambayo yangeweza kukingwa. Matukio kama hayo huzingatiwa kutoka mtazamo wa epidemiologia - yanaweza kuepukwa na kukingwa. Maneno yanayopendelewa hueza kulifananua tukio lenyewe zaidi, badala ya asili yake isiyotakikana (k.m kugongana, kufa maji, kuanguka, n.k)


Ajali ya aina ya kawaida (magari, moto, nk) huchunguzwa ili kubaini jinsi ya kuepukana nazo katika siku zijazo. Mara nyingine hii hujulikana kama Uchambuzi wa sababu ya asili, lakini haihusu ajali ambazo haziwezi kutabiriwa. Sababu haswa ya ajili ya nadra isiyoweza kuepukwa huenda ikawa haiwezi tambulika, na kwa hivyo matukio ya siku zijazo zitabaki kuwa "ajali."

Ufafanuzi

Unapofafanua kinaganaga, ajali huweza kutaja tukio lenyewe pekee, bila kuzingatia mazingira ya tukio hilo, au athari za tukio hilo, yaani "ajali" huishia katika tukio la mara moja, ambalo huleta athari ambazo hazikutarajiwa. Katika matumizi ya kawaida, hata hivyo, 'ajali' huenda ni pamoja na mfumo mzima wa mazingira (fursa, iliyokuwepo awali, au matokeo yanayojiendeleza bila kuthibitishwa; matokeo ya kawaida; wakati na mahali yasiyoweza kutabiriwa; washiriki; nk) yanayoelekea, pamoja na, kusababishwa na tukio hilo.

Aina

Kimaungo na yasiyo ya kimaungo

Mifano ya kimaungo ni kama, migongano isiyotarajiwa au maanguko, kujeruhiwa kwa kugusa kitu kali, moto, au umeme, au kunywa sumu. Mifano ya ajali isiyo ya kimaungo ni kama, kutoboa siri bila kutaka au kusema kitu kimakosa, kusahau miadi, nk


Katika Shughuli

  • Ajali wakati wa utekelezaji wa kazi huitwa ajali kazini.
  • Kwa kulinganisha, ajali zinazotupata tukibarizi au tunapostarehe huwa sanasana ni majeraha ya michezo.


Kwa gari

Sababu za kawaida

Matukio ya ajali, yakibainishwa kwa shughuli.

Kwa majeraha ya kimwili yanayopeleka watu kulazwa hospitalini, nyingi huwa ni ajali za barabara na kuanguka.

Tazama pia


Viungo vya Nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: