Faial
Mandhari
Faial ni kisiwa cha funguvisiwa la Azori (kwa Kireno: Ilhas dos Açores - Visiwa vya vipanga) ambalo ni jimbo la kujitawala la Ureno ingawa liko katika Atlantiki takriban km 1,500 magharibi ya Ulaya na 3,600 mashariki ya Amerika ya Kaskazini.
Visiwa vyote ni vya asili ya kivolkeno; hali halisi ni vilele vya milima mirefu sana vinavyotoka nje ya maji kutoka sakafu ya bahari. Milima hii ya kivolkeno ni sehemu ya mgongo kati wa Atlantiki yanapokutana mabamba ya gandunia ya Amerika ya Kaskazini na Afrika.
Visiwa viligunduliwa na mabaharia Wareno mwaka 1427: vilipatikana bila wanadamu. Wakazi wa kwanza walifika kutoka Ureno mwaka 1439.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Azores Info Ilihifadhiwa 9 Januari 2016 kwenye Wayback Machine.