Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Kisiwa cha Norfolk

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Norfolk Island
Territory of Norfolk Island
Bendera ya Norfolk Island Nembo ya Norfolk Island
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: "Inasmuch"
Wimbo wa taifa: Advance Australia Fair (Sogea mbele Australia nzuri)
Lokeshen ya Norfolk Island
Mji mkuu Kingston
°′  °′ 
Mji mkubwa nchini Burnt Pine
Lugha rasmi Kiingereza
Serikali
Mkuu wa Dola
Afisa Mtendaji
Waziri wa kwanza
Eneo la ng'ambo la Australia
Elizabeth II wa Uingereza
Grant Tambling
David Buffett
Madaraka ya kujitawala
Sheria ya Norfolk

1979
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
34.6 km² (ya 226)
0
Idadi ya watu
 - 2004 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
1,841 (ya 232)
53.2/km² (ya 191)
Fedha Dollar ya Australia (AUD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
NFT (Norfolk Island Time) (UTC+11:30)
(UTC)
Intaneti TLD .nf
Kodi ya simu +6723

-



Mahali pa Norfolk

Kisiwa cha Norfolk ni eneo la ng'ambo la Australia katika Pasifiki ya Kusini kati ya Australia, New Zealand na Kaledonia Mpya.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Kisiwa kipo takriban 1500 km upande wa mashariki ya Australia. Pamoja na visiwa vidogo jirani vya Nepean na Phillip ni ya asili ya kivolkeno hivyo kuna ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kisiwa kiliwahi kukaliwa na Wapolynesia jinsi inavyoonekana kwa mabaki ya kijiji kilichogunduliwa na waakiolojia na kuwepo kwa panja na ndizi ambazo zilisambazwa na Wapolynesia kwenye visiwa vya Pasifiki.

Lakini wakati wa kufika kwa nahodha Mwingereza James Cook mwaka 1774 kisiwa kilikuwa bila watu. Cook alikipa jina la Norfolk kwa heshima ya kabaila Mwingereza fulani aliyeitwa hivyo.

Kuanzia 1788 kisiwa kikakaliwa na wafungwa kutoka magereza ya Uingereza na Australia. Lakini majaribio haya yameachwa tena na makambi ya wafungwa kuhamishwa penginepo.

Mwaka 1856 mababu wa kwanza wa wakazi wa leo walifika kutoka Pitcairn. Idadi ya wajukuu wa waasi wa Bounty ilikuwa imeongezeka mno kwa kisiwa kidogo na serikali ya Uingereza iliwahamisha watu 194 kwenda Norfolk.

Leo hii theluthi moja ya wakazi wa Norfolk ni wa asili ya Pitcairn. Wengine wamekuja kutoka Australia au kutoka Polynesia.


Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.