Nanga
Nanga ni kifaa cha kushikilia meli au boti mahali pamoja ikikaa kwenye maji isiyo na kina kubwa mno lakini mbali na ufuko kiasi haiwezi kufungwa kwa kamba ufukoni.
Nanga inashika meli kutokana na uzito wake au pia kwa msaada wa umbo lake. Linafungwa kwenye nyororo na kushushwa katika maji hadi kufikia chini. Tendo hili huitwa kutia nanga. Hapa inajishikilia kwenye miamba au mchanga wa chini kwa meno yake. Meli ikitaka kuondoka nanga huvutwa juu kwa njia ya nyororo yake.
Hivyo ni kifaa muhimu cha usalama wa meli.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Nanga za kwanza zilikuwa miamba tu zilizofungwa kwa kamba na zinatumiwa hadi leo kwa maboti au jahazi ndogo.
Nanga iliyoboreshwa ilikuwa na mikono miwili mikali ya ubao iliyofungwa pamoja na mwamba kusudi izame chini. Uzito wa mwamba ulizamisha nanga yote na mikono kujishikilia kwenye miamba au mchanga wa chini.
Kiasi jinsi meli zilivyokuwa kubwa nanga ilitakiwa kuwa imara zaidi hivyo nanga za chuma na feleji zimezidi kuwa kawaida. Umbo la nanga limebadilika mara kwa mara pamoja na maarifa na teknolojia. Siku hizi mara nyingi nanga yenye umbo la jembe la kukunjwa hupendelewa.
Vifaa vya nanga
[hariri | hariri chanzo]Nanga yenyewe inaenda sambamba na nyororo yake. Boti ndogo zinanendelea kutia nanga zinazoshikwa kwa kamba. Lakini kwa meli kubwa uzito wa nyororo ni sehemu muhimu ya uwezo wa nanga. Nyororo hutolewa kulingana na kina cha maji kiasi cha kuwa na mita nyingi za nyororo za kulala chini zinazozidi kina cha maji kabla ya kuelekea kwa meli yenyewe. Nyororo nzito ya kulala chini inapunguza nguvu inayovuta kwenye nanga yenyewe wakati meli ina mwendo kulingana na mawimbi.
Nyororo hizi zinahitaji winchi kubwa kwenye meli inayozungushwa kwa nguvu ya injini.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- "Ultimate Holding Power" - Anchor Test Archived 27 Machi 2009 at the Wayback Machine. from Yachting Monthly Desemba 2006
- "Holding Power" - 14 Anchors Tested Archived 27 Machi 2009 at the Wayback Machine. from SAIL magazine Oktoba 2006
- Lightship anchors Archived 27 Septemba 2007 at the Wayback Machine.
- About the Manson Supreme Anchor — Article discussing problems with copies of genuine anchor types
- A Process of Evolution — An essay on boat anchors by New Zealand boatbuilder, offshore cruiser, & consultant Peter Smith
- The Bottom Line: Anchoring In 2007 — Article on anchoring from Coastguard Member's Handbook 2007