Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Visiwa vya Virgin vya Uingereza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 14:45, 29 Novemba 2023 na SpesBona (majadiliano | michango) (+ {{Amerika Kaskazini}})
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Ramani ya Visiwa vya Virgin vya Uingereza

Visiwa vya Virgin vya Uingereza (British Virgin Islands) ni funguvisiwa katika Bahari ya Karibi karibu na Puerto Rico ambavyo ni eneo la ng'ambo la Uingereza. Wakazi ni raia wa Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini lakini hawashiriki katika uchaguzi wa bunge la London.

Katika sehemu hii ya nyororo ya Visiwa vya Bikira (Virgins) kuna visiwa 16 vyenye wakazi na zaidi ya 30 visivyo na watu. Eneo lake ni km² 153.

Idadi ya wakazi hufikia takriban 22,000. Wengi wao (85-90%) ni wa asili ya Kiafrika; mababu wao walikuwa watumwa kutoka Afrika waliopelekwa visiwani kufanya kazi kwenye mashamba ya miwa.

Visiwa vikubwa ni Tortola, Virgin Gorda, Anegada na Jost Van Dyke. Mji pekee na makao makuu ya kiutawala ni Road Town kwenye kisiwa cha Tortola.

Uchumi hutegemea zaidi utalii. Menginevyo kuna ushirikiano wa kiuchumi na sehemu ya Kimarekani ya visiwa vya Virgins na pesa inayotumika hata upande wa Kiingereza ni dola ya Marekani.

Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Visiwa vya Virgin vya Uingereza kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.