Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Altava

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Algeria, ilipo Altava

Altava ulikuwa mji wa Dola la Roma wenye mchanganyiko wa Warumi na Waberberi nchini Algeria.

Uliwahi kuwa mji mkuu wa Ufalme wa kale wa Waberberi wa Altava. Kwa mujibu wa mwanahistoria aitwaye Lawless, mji wa Altava ulipata uhuru kutoka kwa ngome ya kijeshi ya eneo hilo,na ulikuwa na jumba kubwa na hekalu muhimu la Kipagani ambalo baadaye lilibadilishwa kuwa kanisa la Kikristo. Hii ilikuwa ni dalili iliyoonesha ongezeko la Ukristo katika jamii ya Waberberi. Makazi hayo ya kirumi yalikuwa na eneo la takribani hekta 13 na yalizungukwa na mashamba.[1]

  1. Lawless, R. Mauretania Caesartiensis: anarcheological and geographical survey Section: The Roman Civilian Sites. p.122-195
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Altava kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.