Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Teleka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Apodidae)
Teleka
Teleka mweusi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Apodiformes (Ndege kama teleka)
Familia: Apodidae (Teleka)
Hartert, 1897
Ngazi za chini

Nusufamilia 2 na enasi 29:

Teleka au barawai ni ndege wa familia Apodidae. Ndege hawa ni wadogo wenye mabawa marefu kwa umbo wa mundu. Rangi yao ni kahawia au kijivu na mara nyingi kiuno, koo na/au tumbo ni nyeupe. Teleka hupitisha takriban maisha yao yote angani wakikamata wadudu. Kwa hivyo ndege hawa hawawezi kutembea vizuri. Zamani watu walifikiri kwamba teleka hawana miguu, wakawapatia jina “apus” kutoka Kiyunani α = bila na πους = mguu. Hunywa pia wakiruka, lakini hulala wakishika nyuso ya wima.

Teleka hujenga tago lao kwa vitu mbalimbali (vitawi, maua, majani, nyuzi, manyoya, wadudu) ambavyo vinagundishwa pamoja na mate. Matago ya spishi nyingine yamejengwa kwa mate pekee na haya yalika, huko Uchina hasa. Jike huyataga mayai 1-4.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine

[hariri | hariri chanzo]

Spishi za kabla ya historia

[hariri | hariri chanzo]
  • Aerodramus manuoi (Mangaia Swiftlet, Holocene, Mangaia)
  • Apus gaillardi (Kati hadi mwisho wa Miocene, La Grive-St.-Alban, Ufaransa
  • Apus wetmorei (Mwanzi hadi mwisho wa Pliocene, Ulaya ya Kati)
  • Apus baranensis (Mwisho wa Pliocene, Ulaya Kusini Mashariki)
  • Apus submelba (Kati ya Pleistocene, Slovakia)
  • Chaetura baconica (Mwisho wa Miocene, Hungaria)
  • Collocalia buday (Mwanzo wa Miocene, Riversleigh, Australia)
  • Tachornis uranoceles (Mwisho wa Pleistocene, Puerto Rico)