Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Basi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Basi dogo huko Novoaltaisk.
Basi la masafa marefu huko Krakow, Polandi.

Basi (kutoka Kiingereza "bus") ni chombo cha usafiri kinachotumika kusafirisha watu kutoka eneo moja kwenda eneo jingine kwa ajili ya shughuli mbalimbali, kwa mfano kazi, masomo, utafiti na kadhalika.

Vyombo hivi vipo vya aina mbalimbali, kwa mfano kuna mabasi madogo yanayobeba abiria wachache na kusafiri umbali wa kawaida, pia kuna mabasi makubwa yenye kubeba watu wengi kuanzia hamsini na kuendelea na mabasi hayo husafiri umbali mrefu: yanaweza kusafiri kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine bila kumpumzishwa.

Katika dunia ya sasa mabasi yanatumika sana katika shughuli mbalimbali, kwa mfano shughuli za kiuchumi kwa kusafirisha wafanyakazi na wafanyabiashara katika nchi mbalimbali.

Kwa msaada wa vyombo hivyo watu wanaweza kufika sehemu nyingi kwa wakati na kwenye kazi zao kwa wakati; hali hii imesaidia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa nchi nyingi duniani.

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.