Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Bendera ya Poland

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Poland
Bendera ya Poland pamoja na nembo la kitaifa

Bendera ya Poland ni ya milia miwili ya kulala yenye rangi za nyeupe na nyekundu. Mlia mweupe uko upande wa juu, mlia mwekundu uko chini.

Bendera ilianzishwa kwa azimio la Bunge la Poland mwaka 1831. Rangi hizi mbili zilipatikana katika nembo ya nchi tangu karne tisa ikionyesha tai nyeupe juu ya rangi nyekundu.

Bendera za kufanana

[hariri | hariri chanzo]

Bendera ileile inapatikana Bohemia (ni sehemu ya Uceki), Thuringia (jimbo la Ujerumani) na Kantabria (jimbo la Hispania). Bendera zinazofanana ziko Monako, Indonesia na Solothurn (jimbo la Uswisi) (rangi zilezile lakini mlia mwekundu uko juu).