Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Boutros Boutros-Ghali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Boutrous Boutrous-Ghali

Boutros Boutros-Ghali (Kar. بطرس بطرس غالي, Kikopti: Bουτρος Βουτρος-Γαλι) (alizaliwa 14 Novemba 1922 - 16 Februari 2016) alikuwa mwanasiasa na mtaalamu wa sheria kutoka nchini Misri. Alikuwa katibu mkuu wa Umoja wa KimataifaUN kati ya 1992 na 1996.

Alizaliwa katika familia ya Wakristo Wakopti mjini Kairo. Babu yake alikuwa waziri mkuu wa Misri. Baada ya shule alisoma sheria kwenye chuo kikuu cha Kairo akamaliza 1946 akaendelea kuchukua shahada ya udaktari huko Ufaransa.

Baada ya kufunza miaka kadhaa alipewa nafasi ya naibu waziri wa maswala ya kigeni chini ya rais Anwar as-Sadat. Akishughulika amani kati ya Israeli na Misri alisaidia pia kutiwa huru kwa aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela.

Kuanzia Januari 1992 hadi Januari 1997 alikuwa Katibu Mkuu wa UM, akiwa Mwafrika wa kwanza kwenye nafasi hii.