Buku
Mandhari
Buku | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Buku-misitu (Cricetomys emini)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Mabuku ni wanyama wa nusufamilia Cricetomyinae katika familia Nesomyidae ambao wanafanana na panya, lakini panya ni wanafamilia wa Muridae. Mabuku ni wakubwa kiasi, pengine kushinda panya: wale wa Cricetomys wana mwili wa sm 25-45, mkia wa sm 36-46 na uzito wa kg 1-1.5; wale wa Beamys wana mwili wa sm 13-19, mkia wa sm 10-16 na uzito wa g 55-150; na wale wa Saccostomus wana mwili wa sm 9.5-19, mkia wa sm 3-8 na uzito wa g 40-120. Wana pochi kwa ndani ya mashavu yao ambazo wazitumia kwa kuweka chakula. Hula mbegu, matunda, makokwa, mizizi na wadudu na hupenda machikichi sana. Rangi yao ni kijivu au kahawia juu na nyeupe chini.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Beamys hindei, Buku Mkia-mrefu Mdogo (Lesser Hamster-rat au Long-tailed Pouched Rat)
- Beamys major, Buku Mkia-mrefu Mkubwa (Greater Hamster-rat au Greater Long-tailed Pouched Rat)
- Cricetomys ansorgei, Buku Kusi Southern giant pouched rat) – mara nyingi inaainishwa kama nususpishi ya C. gambianus
- Cricetomys emini, Buku-misitu (Emin's pouched rat)
- Cricetomys gambianus, Buku Kaskazi (Gambian pouched rat)
- Cricetomys kivuensis, Buku wa Kivu (Kivu giant pouched rat) – mara nyingi inaainishwa kama nususpishi ya C. emini
- Saccostomus campestris, Kibuku Kusi (South African pouched mouse) – yumkini mchanganyiko wa spishi
- Saccostomus mearnsi, Kibuku Mashariki (Mearns's pouched mouse) – yumkini mchanganyiko wa spishi
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Buku kaskazi
-
Kibuku kusi