Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Chuo Kikuu cha Moi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Moi


Chuo Kikuu cha Moi ni chuo kikuu mjini Eldoret, magharibi mwa Kenya. Ni mojawapo wa taasisi saba za elimu ya juu za kitaifa, zingine zikiwa Chuo Kikuu cha Nairobi, Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta cha Kilimo na Teknolojia, Chuo Kikuu cha Maseno University, Chuo Kikuu cha Egerton, Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Kimathi na Chuo Kikuu cha Kenyatta. Kilianzishwa mwaka wa 1984 na Sheria ya Bunge ya Chuo Kikuu cha Moi kufuatia mapendekezo ya Tume ya Mackay. Hadi mwaka wa 2007 kilikuwa na wanafunzi zaidi ya 20,000, 17,086 walikuwa wanafunzi wa shahada, na kina matawi 8 ya vyuo vyake pamoja na vyuo viwili vya kiufundi.

Chuo kinasisitiza sayansi na teknolojia kuliko sanaa. Kina shule zifuatazo:

  • Shule ya Kilimo na Teknolojia Hai
  • Shule ya Uchumi na Usimamizi wa Biashara
  • Shule ya Elimu
  • Shule ya Sayansi ya Habari
  • Shule ya Uhandisi
  • Shule ya Sayansi
  • Shule ya Usimamizi wa Mali Asili
  • Shule ya Utabibu
  • Shule ya Utabibu wa Meno
  • Shule ya Afya kwa Umma
  • Shule ya Sheria
  • Shule ya Masomo ya Mazingara
  • Shule ya Sanaa na Sayansi Isimu
  • Shule ya Ukuzaji wa Rasilimali Binadamu

Matawi ya vyuo :

Tawi la Main Campus

Chepkoilel Campus

Town Campuses

Matawi ya Umbali:

  • Nairobi Campus
  • Kitale Campus
  • Kericho Campus
  • Mount Kenya Campus
  • Southern Nyanza Campus

Vyuo vitegemezi

  • Chuo cha Kabianga University College
  • Chuo cha Narok University College

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Moi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.