Ekseli
Mandhari
Ekseli ni nondo au mhimili unaotumiwa kushika gurudumu linalozunguka.
Kuna mitindo miwili ya kuweka ekseli:
- ekseli imara isiyozunguka na hapo gurudumu inafungwa kwenye ncha za ekseli. Msuguano kati ya ekseli na gurudumu unahitaji kupungukiwa ama kwa kuweka mafuta nchani ya ekseli au kwa kufunga beringi kati ya gurudumu na ekseli.
- ekseli inayozunguka inafungwa moja kwa moja kwenye gurudumu na hapo ekseli yenyewe inazunguka na hapo beringi inahitaji kuwekwa mahali ambako ekseli yenyewe inafungwa.