Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Elimu ya juu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chuo Kikuu cha Cambridge ni taasisi ya elimu ya juu.

Elimu ya juu, yaani ile ya baada ya shule ya upili au elimu ya awamu ya tatu, si ya lazima. Elimu hii kwa kawaida hujumulisha viwango vya shahada pamoja na elimu ya ujuzi wa kitaalamu.

Kwa jumla elimu ya juu hutolewa na vyuo na vyuo vikuu na huambatana na kutolewa kwa vyeti, stashahada za diploma na shahada za digrii kitaaluma.

Masomo ya juu hujumuisha elimu, utafiti na huduma za jamii na katika uwanja wa elimu, hujumulisha viwango vya shahada ya kwanza na nyingine za juu. Elimu ya juu aghalabu huhusu kufuzu katika kiwango cha shahada ya kwanza, ya uzamili na ya uzamifu.

Idadi kubwa ya watu katika nchi zilizoendelea (hadi kufikia asilimia 50) wameweza kupata elimu ya juu wakati fulani maishani mwao. Kwa hiyo, elimu ya juu ni muhimu kwa uchumi wa taifa, ni kiwanda cha pekee ambacho huzalisha wafanyakazi walioelimika.

Katika nchi maskini au zenye uchumi wa chini serikali zinatakiwa kuongeza mikopo kwa wanafunzi wa vyuoni ili waweze kupata elimu hiyo na kusonga mbele, kwa kuwa elimu ni ufunguo wa maisha.