Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Hajivale

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hajivale
Hajivale wa Afrika
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Acciptriformes (Ndege kama vipanga)
Familia: Accipitridae (Ndege walio na mnasaba na vipanga)
Nusufamilia: Polyboroidinae (Hajivale)
Jenasi: Polyboroides
A. Smith, 1829
Ngazi za chini

Spishi 2:

Hajivale au kobeamiti ni ndege mbua wa jenasi Polyboroides, jenasi pekee ya nususfamilia Polyboroidinae katika familia ya Accipitridae. Manyoya yana rangi ya majivu na chini yao ni nyeupe yenye milia myembamba kijivu; mkia ni mweusi mwenye baka jeupe moja au mabaka meupe mawili. Wana kiraka cha upara pande zote za macho isipokuwa hajivale wa Amerika.

Ndege hawa hula wanyama na ndege wadogo, nyoka, mijusi, vyura na wadudu, na hajivale wa Afrika na Madagaska hula machikichi pia. Wanaweza kupanda miti na kukamata makinda ya zuwakulu au goregore ndani ya matundu ya hawa kwa miguu mirefu yao. Hulitengeneza tago lao kwa vijititi juu ya mti na jike huyataga mayai 1-3. [onesha uthibitisho]