Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Jens Fink-Jensen

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jens Fink-Jensen. Ideogramma International Literature Festival in Nicosia, Cyprus, 27.11.2019.
Jens Fink-Jensen. Ideogramma International Literature Festival in Nicosia, Cyprus, 27.11.2019.

Jens Fink-Jensen (alizaliwa Copenhagen, Denmark, 19 Desemba 1956) ni mwandishi katika lugha ya Kidenishi katika nyanja mbalimbali kama vile semi za kawaida na mashairi. Vile vile yeye ni mpigapicha na mwandishi wa vitabu hasa vya muziki na nyimbo.

Alianza maisha yake kama mwandishi wa vitabu vya hadithi 4 Juni 1975 wakati alipoandika hadithi fupi ijulikanayo kama Juni 1995. Kitabu hicho kilichapishwa kwenye gazeti la kila siku kwa lugha ya Kidenish lijulikanalo kama "Nipashe Habari'". Hatimaye kwenye mwezi wa Mei katika mwaka wa Elfu Moja na Mia Tisa na Sabini na Sita, akawa mwandishi wa mashairi kwanza kwa kuandika tunzi nne za mashairi zilizo chapishwa kwenye jarida nambari sabini na sita mkwaju moja, na ambalo hujulikana kama “Mbegu ya Ngano” (Hvedekorn).

Tunzi zake za mwanzo kwenye nyanja ya mashairi zilichapishwa kwa mara ya kwanza kunako Mwaka wa Elfu Moja Mia Nane na Dhemaanini na Moja na zikajulikana kwa kupewa kicwa cha maneno Dunia Kwenye Jicho. Alianza kukusanya mashairi yalio kua yameandikwa na washairi wengine na kuyaweka katika hali ya vitabu kwenye mwaka wa Elfu Moja Mia Tisa na Dhemanini na Sita. Vitabu vyenyewe vilichapishwa vikiwa katika hali ya mkusanyiko wa hadidhi fupi-fupi na vikatambulika kwa jina la Wanyama mwitu. Hatimae kunako mwaka wa Elfu Moja Mia Tisa na Tisini na Nne, akaanza kuandika vitabu kwa watoto, baadhi yavyo kikiwa ni kile kiitwacho Jonas na Konokono.

Alihitimu masomo yake kwenye shule ya upili kidato cha sita na kupita vizuri katika masomo ya lugha mbali-mbale akiwa katika shule ya bweni ya Herlufsholm kunako mwaka wa Elfu Moja mia Tisa na Sabini na Sita. Baadae alifanya mafunzo ya kijeshi na kuhitimu kwa kutunukiwa cheo cha Kamanda kwenye kikosi kiitwacho Walinzi Hai wa Kifalme (Royal Life Guards). Hatimae kwenye mwaka wa Elfu-moja na Mia Tisa na Dhemaanini na Sita, akajiunga na chuo kitoacho masomo kwenye fani ya ujenzi kilichoko mjini Conpenhagen amboko alitunukiwa shahada ya Mastas katika uchoraji na ujenzi. Katika mwaka wa Elfu moja Mia Tisa na Tisini na Saba, akiwa bado angali kwenye chuo hicho-hicho, aliyaendeleza masomo yake kwa kushiriki kwenye masomo ya ukusanyaji na utoaji wa habari katika misingi inayo husisha matumizu ya mbinu mbali-mbali.

Na akiwa kama mojawapo wa waandishi wakongwe walio vuma katika miaka ya Dhemaanini na ambao walipenda kua na uhusiano wa karibu sana na bwana Poul Borum, (mhariri wa Hvedekorn), yeye pamoja na wenzake wengine kama vile Michael Strunge, walichangia katika kubuni onyesho la kusisimua ambalo lilijulikana kama “Kizazi Kipya” na ambalo liliandaliwa katika ukumbi wa Huset ulioko mjini Copenhagen. Hii ilikua ni kwenye mwaka wa Elfu Moja mia Tisa na Dhemaanini.

Vile-vile, alijishirikisha kwenye maonyesho ya tunzi mbali-mbali na alishikilia nafasi maalum ya kusoma mashairi yenye kuelezea hali ya furaha na huzuni, huku akionyesha picha zinazo onyeshwa kwenye kuta kwa kutumia miale ya mwangaza. Mengine alio jihusisha nayo yalikua ni Kuleta hali ya uuwiyano katika tunzi mbali-mbali zilizo tungwa na shule mbali-mbali za upili, na kwenye sherehe zingine mbali-mbali zilizo wahi kufanyika wakati huo; Hii ikiwa ni baadhi ya matukio mengine alio jihusisha nayo. Wengine walio shiriki nae ni mwana mziki Fredrik Mellqvist ambae ana uhodari wa kucheza chombo kiitwacho Keyboard. Wengine alio shiriki nao ni pamoja na yule mchezaji wa chombo kiitwacho Saksafoni aitwae Jens Severin.

Mwana sanaa huyu Jens Fink-Jensen amewahi vile-vile kuandaa maonyesho ya picha, kwamfano yale yaliyo julikana kama “Meli za Kusini” pamoja na Uso wa Beijing. Mengine yalikua ni pamoja na maonyesho yalio julikana kama Picha za Neno ambazo ziliandamana na picha ambazo huonyeshwa kwa kutumia miyale ya mwangaza na ambazo hushirikisha sauti. Mfano ukiwa ni ile ijulikanayo kama Jicho limulikalo Ulimwengu likiwa ni onyesho lililokua linasimulia kuhusu malighafi inayo tumika ndani ya vitabu.

Orodha ya vitabu vingine alivyowahi kuchapisha

[hariri | hariri chanzo]
  • 1981 Mashairi ya Verden i et øje (Dunia kwenye jicho)
  • 1982 Mashairi ya Sorgrejser (Safari za kufadhaisha)
  • 1983 Mashairi ya Dans under galgen (Kucheza densi kwenye miti ya kunyongea watu)
  • 1986 Hadidhi Fupi za Bæsterne (Wanyama mwitu)
  • 1988 Mashairi ya Nær afstanden (Karibu ya mwendo) (yalio chapishwa kwa lugha ya Kiarabu 1999)
  • 1994 Vitabu kwa Watoto Jonas og konkylien (Jonas na konokono) (ambamo picha za tafsiri zimechorwa na msanii Mads Stage)
  • 1995 Mashairi ya Forvandlingshavet (Bahari ya mageuzi).
  • 1998 Kitabu Kwa Watoto Jonas og himmelteltet (Jonas na hema ipepeayo kwenye mawingu) (ambamo picha za tafsiri zimechorwa na msanii Mads Stage)
  • 2002 Mashairi ya Alt er en åbning (Kila kitu ni ufunguo mpya)
  • 2005 Chaguo Maalum la Mashairi Mia Moja ya kimapenzi ya Syd for mit hjerte (Kusini ya moyo wangu)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]