Jimbo Katoliki la Lodi
Mandhari
Jimbo katoliki la Lodi (kwa Kilatini "Dioecesis Laudensis") ni mojawapo kati ya majimbo 223 ya Kanisa Katoliki nchini Italia na kama hayo yote (isipokuwa 3) linafuata mapokeo ya Kiroma.
Kikanisa linahusiana na Jimbo Kuu la Milano.
Askofu wake ni Maurizio Malvestiti.
Historia
[hariri | hariri chanzo]- 378: Kanisa la kwanza kuwekwa wakfu katika Laus Pompeia kutoka San Bassiano
- 4 Novemba 1163: Kufanywa dayosisi
Uongozi
[hariri | hariri chanzo]- Maaskofu wa karne ya 20
- Giovanni Battista Rota † (1888 - 1913)
- Pietro Zanolini † (1913 - 1923)
- Ludovico Antomelli, O.F.M. † (1924 - 1927)
- Pietro Calchi Novati † (1927 - 1952)
- Tarcisio Vincenzo Benedetti, O.C.D. † (1952 - 1972)
- Giulio Oggioni † (1972 - 1977)
- Paolo Magnani (1977 - 1988)
- Giacomo Capuzzi (1989 - 2005)
- Giuseppe Merisi (2005 - 2014)
- Maurizio Malvestiti, kutoka 26 Agosti 2014
Takwimu
[hariri | hariri chanzo]Eneo ni la kilometa mraba 894, ambapo kati ya wakazi 286.469 (2012) Wakatoliki ni 272.900 (95,3%).