Karakana
Karakana ni chumba cha kuweka magari wakati hayatumiki. Neno hili pia laweza kutumika kumaanisha mahala magari hutengenezewa wakati yana shida fulani. Neno la Kiingereza la karakana ni garage.
Karakana za nyumbani huenda zikawa zimeambatanishwa na chumba cha kukaa au kikawa ni chumba kilicho kando ya chumba kinachoishiwa na watu. Kwa kawaida, karakana huwa na lango kubwa ili kuwezesha gari kuingia au hata kutoka kwa urahisi. Lango hili kwa kawaida hufunguka kwa juu.
Kwa kawaida, karakana huwa na nafasi ya kuhifadhi gari moja, mbili au hata tatu kulingana na zile alizonazo mwenye karakana. Karakana husaidia kwa kuhifadhi gari lisiharibike kwa kunyeshewa, kupatwa na jua kali na pia kuibwa.
Kufuli za karakana huweza kufunguliwa bila kutumia ufunguo wa kawaida. Kufuli hizi hufunguliwa kwa kubofya nambari kwa kibodi au hata kwa kutumia rimoti. Nambari hizi huwa kama nywila ambazo mwenye karakana huhakikisha hazijulikani na wengine. Maana ya kutokuwa na ufunguo wa kawaida ni kwamba mwenyewe aweze kuingia kwa urahisi bila hata kutoka katika gari lenyewe.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |