Kariba, Zimbabwe
Majiranukta: 16°31′0″S 28°48′0″E / 16.51667°S 28.80000°E | |
Country | Zimbabwe |
---|---|
Province | Mashonaland West |
District | Kariba District |
Idadi ya wakazi (2012) | |
- Wakazi kwa ujumla | 26,451 |
CET | (UTC+1) |
- Summer (DST) | CEST (UTC+1) |
Kariba ni mji wa mkoa wa Mashonaland Magharibi, Zimbabwe, ulioko karibu na Bwawa la Kariba katika eneo la mwisho wa Ziwa Kariba, karibu na mpaka wa Zambia. Kulingana na matokeo ya sensa ya mwaka 2012, mji huu ulikuwa na idadi ya wakazi 26,451.
Ukiwa katika Bonde la Zambezi, mji wa Kariba una joto mwaka mzima.
Kariba ni kiungo cha kati katika sekta ya utalii kwenye kanda ya Ziwa Kariba. Mji Kariba unatoa mahala pa kupumzika kwenye mahoteli na vyumba vya kulala. Mnamo mwaka 2006, ni hoteli tatu tu zilizokuwa wazi. Kuna kasino mbili katika mji huu na mikahawa kadhaa. Vivutio vingi kwa watalii katika Kariba ni vya maji. Uvuvi, kutazama wanyamapori, na mchezo wa ndani wa mashua ni shughuli maarufu zaidi. Ziara katika ukuta wa Lambo la Kariba pia ni ya kuvutia.
Mji huu uliundwa kuwashughulikia wafanyakazi ambao walikuwa wanajenga bwawa katikati na mwishoni mwa 1950. Mamlaka ya Ugawi wa Umeme ya Zimbabwe(Zimbabwe Electricity Supply Authority-ZESA) inaajiri wafanyikazi katika kituo cha nguvu za umeme. Kiwanda cha uvuvi cha Kapenta pia ni sekta muhimu, ingawa kimekuwa kikiathiriwa na uhaba wa mafuta.
Kariba ina vitongoji vikuu vitatu: Mahombekombe,kitongoji cha wakongwe maskini kwenye fuo za ziwa , Nyamhunga kitongoji kipya cha wakazii wengi, na Kariba Heights, kitongoji cha ndani cha matajiri na nyumbani kwa jimbo la kumbukumbu la Operation Noah. Kariba Heights kama vile jine lake linaashiria kiko milimani na kutazama Ziwa Kariba kutoka milima hii inapendeza sana.
Mji huu una shamba la mamba na uwanja wa ndege, kwa safari za ndege hadi Victoria Falls na Harare.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- "Kariba Information" Archived 27 Septemba 2007 at the Wayback Machine.. Realtravel.com. Ilir
- "Kariba, Zimbabwe" Archived 17 Juni 2011 at the Wayback Machine.. Travelpost.com. ilirudishwa 13 Agosti 2008.
- "Kariba Culture" Archived 27 Septemba 2011 at the Wayback Machine.. Africatravelling.net. ilirudishwa 13 Agosti 2008.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kariba, Zimbabwe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |