Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Kidudu-dubu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kidudu-dubu
Picha ya kidudu-dubu kwa hadubini ya elektroni
Picha ya kidudu-dubu kwa hadubini ya elektroni
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila ya juu: Ecdysozoa (Wanyama wanaoambua kiunzi cha nje]]
Faila: Tardigrada (Wanyama wenye )
Ngazi za chini

Ngeli, oda na familia

Vidudu-dubu (kutoka Kiholanzi beerdiertjes) ni viumbehai vinavyofanana na dubu wadogo sana wenye jozi nne za miguu; wengi zaidi wana mm 0.3-0.5 wakiwa wazima, lakini kuna spishi kadhaa za hadi mm 1.2 na nyingine za mm 0.1 tu. Wanatokea katika maji au mahali pa majimaji. Wanyama hawa wanaweza kuendelea kuishi katika hali za kuzidi kiasi: kutoka halijoto ya karibu na sifuri halisi hadi juu ya kiwango cha kuchemka, ukavu kabisa, kanieneo kubwa sana, ombwe kabisa na mnururisho kali unaoionisha. Wakikaa katika hali ya ukavu kabisa, hupoteza takriban maji yote mpaka kubaki na 3% tu na hata baada miaka kumi katika hali hii wanaweza kuamka na kuendelea kuishi.

Makala hii kuhusu "Kidudu-dubu" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili beerdiertje kutoka lugha ya Kiholanzi. Neno (au maneno) la jaribio ni kidudu-dubu.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.