Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Kinahuatl

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kinahuatl (nāhuatl, mexìcatlàtōlli) ni kati ya lugha asilia za Mexiko zilizopo tangu wakati kabla ya kufika kwa Wahispania. Idadi ya wasemaji wa lahaja zake ni takriban milioni moja na nusu.

Ilikuwa lugha ya Waazteki, Watolteki na wengine wa nyanda za juu za Mexiko. Tangu kufika kwa ukoloni lahaja mbalimbali zilijitokeza si wasemaji wote wanaoelewa wasemaji wote wengine.

Maneno ya Nahuatl yalitaja mazao yaliyopelekwa kote duniani pamoja na majina yao. Kati ya maneno ya Nahuatl yaliyosambaa duniani ni:

Majina ya nchi za Mexico, Guatemala na Nikaragua yana asili za Nahuatl.