Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Kodi (ushuru)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Fomu ya malipo ya kodi

Kodi (pia: ushuru) ni malipo ambayo watu wanatozwa na serikali.

Kusudi la kodi

[hariri | hariri chanzo]

Kodi ni chanzo kuu cha mapato kwa serikali ya kisasa. Mapato haya yanagharamia shughuli za serikali, mishahara na marupurupu za watumishi wa dola, gharama za huduma zinazotolewa na serikali au za shughuli za umma: kwa mfano shule, hospitali, ujenzi wa barabara, polisi, mahakama au jeshi.

Aina za kodi

[hariri | hariri chanzo]

Kuna njia mbalimbali za kutoza kodi

  • kodi ya moja kwa moja kutoka wananchi (mfano: kodi ya mapato - kila mtu mwenye mapato hutozwa asilimia fulani kulingana na jumla ya mapato yake)
  • kodi isiyo dhahiri kupitia bei za bidhaa au huduma (mfano:kodi ya mauzo - bidhaa zinaongezwa kodi ya mauzo kulingana na asilimia ya bei ya bidhaa na kiasi hiki huongezwa juu ya bei kwa hiyo ni wateja wanaolipa kodi kupitia bei)
  • kodi zinazotegemea mali ya watu kwa mfano kodi kwa nyumba au eneo lake au shamba.

Siku hizi kodi hutozwa kama pesa lakini kihistoria na katika mazingira ambako watu hawana pesa taslim kodi inatolewa pia kwa njia ya kazi. Mfano ni ujenzi wa barabara ambako wananchi wote wa eneo fulai wanapswa kushiriki na kuchangia kazi yao kwa muda fulani.

Katika mazingira ya mashambani zamani kodi ililipwa pia kwa kutozwa asilimia ya mavuno au mifugo.

Kukusanya kodi

[hariri | hariri chanzo]

Malipo ya kodi ni wajibu wa wananchi hata kama watu wengi wanajaribu kuepukana nayo. Serikali inadai malipo ikitisha adhabu kwa watu wanaoficha mapato yao au wanaokataa malipo.

Serikali huwa na idara za kodi ambazo zimekabidhiwa jukumu la kutunza kumbukumbu ya malipo na kukusanya pesa zinazodaiwa.

Katika mazingira ya kisasa ni makampuni yanayopaswa kukusanya kodi za wafanyakazi kwa njia ya kukata kodi kwenye mshahara na kuzikabidhi kwa serikali.

Biashara zinatakiwa kutunza kumbukumbu za mapato kwa kodi isipokuwa mara nyingi biashara ndogondogo hutozwa kiasi fulani isiyobadilika bila kuchunguza mapato yenyewe.

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kodi (ushuru) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.