Litania
Mandhari
Litania ni aina ya sala ya Ukristo ambayo upekee wake ni kuwa na mfululizo wa maneno ya sifa na maombi ambayo yanaitikiwa na mkusanyiko kwa namna iliyopangwa, kwa kawaida ya kujirudiarudia.
Jina linatokana na neno la Kigiriki λιτανεία (litaneía), linalotokana na λιτή (litê), yaani "dua".
Mtindo huo wa kusali ulistawi kuanzia Antiokia ukaenea kwanza Mashariki halafu Mashariki hasa katika karne IV.
Mfano wa litania fupi katika liturujia ni Mwanakondoo wa Mungu inayotumika katika Misa, na litania ndefu ni litania ya watakatifu inayotumika katika ibada muhimu kadhaa, kama vile upadrisho.