Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Lovre Kalinić

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lovre Kalinić

Lovre Kalinić (alizaliwa 3 Aprili 1990) ni mchezaji wa soka wa Kroatia ambaye anacheza kama kipa wa timu ya taifa na klabu ya Uingereza Aston Villa.

Kazi ya Klabu

[hariri | hariri chanzo]

Hajduk Split

[hariri | hariri chanzo]

Lovre alianza kucheza soka katika klabu ya Kroatia, Hajduk Split akichezea timu ya vijana wadogo na kisha kujiunga na timu kuu ya Hajduk Split. Kwa jumla Hajduk alichezea timu ya vijana na timu kuu Hajduk Split kwa miaka 17[1] akicheza mechi rasmi 134 katika misimu 7.

Ata hivyo akiwa Hajduk aliwahi kuchezea timu kadhaa kwa deni ikiwemo Junak Sinj mwaka wa 2009, Novalja mwaka wa 2010 na Karlovac mwaka wa 2012.

Aliporudi, Hajduk Split, musimu wa 2013-14 aliibuka mlinda lango bora na msimu uliofwata wa 2015-16 aliweka rekodi mpya kama kipa aliyeenda muda mrefu zaidi bila kufungwa bao ligi kuu ya kandanda ya Kroatia (Prva hrvatska nogometna liga kwa kifupi Prva HNL au 1. HNL). Lovre alicheza mechi nane (dakika 775)[2] mbila kufungwa bao akivunja rekodi iliyokuwepo ya dakika 711 iliyoshikiliwa na Zoran Slavica.

Mnamo tarehe 27 Desemba 2016, Lovre Kalinić alikuwa anahamia klabu yake kwanza ya Ubelgiji K.A.A. Gent kwa ada kubwa. Malipo ya uhamisho wake 3.1m ikafanya Kalinić kuwa mchezaji wa gharama kubwa zaidi katika historia ya Gent. Aliweza kuwa kipa bora katika ligi ya Ubelgiji kwa msimu wa mwaka 2016-17.

Aston Villa

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo tarehe 21 Desemba 2018, Kalinic alihamia upande wa uingereza katika klabu ya Aston Villa baada ya kufanya makubaliano na klabu ya Gent mwanzoni mwa Januari.

Alijiunga rasmi 1 Januari 2019. Mechi yake ya kwanza baada ya kufungwa 3-0 kwenye tiketi ya FA Cup dhidi ya klabu Swansea City.

Kazi ya kimataifa=

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya Stipe Pletikosa kustaafu katika soka la kimataifa mwaka 2014, Kalinić akawa kipa namba mbili(2) wa Timu ya taifa ya Kroatia baada ya kipa namba moja (1) Danijel Subašić. Alikuwa sehemu ya kikosi cha Croatia cha UEFA Euro 2016.

Mwezi wa Mei 2018 aliitwa jina lake katika kikosi cha Croatia cha wachezaji 23 kwa ajili ya Kombe la Dunia la FIFA 2018 iliyofanyika nchini Urusi. Baada ya mashindano kumalizika,kipa namba moja Danijel Subašić astaafu katika timu ya taifana Kalinić amechaguliwa kuwa kipa namba moja katika uchaguzi wa timu ya taifa.

  1. "Thank you Lovre and good luck!". hajduk.hr (kwa Kikorasia). Iliwekwa mnamo 2019-06-18.
  2. "Prekinut niz nesavladivosti Lovre Kalinića". Slobodna Dalmacija (kwa Kikorasia). Iliwekwa mnamo 2019-06-18.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lovre Kalinić kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.