Mbangi
Mandhari
Mbangi (Cannabis spp.) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Mbangi (spishi za jenasi Cannabis) ni mmea aina ya vichaka utumikao ili kutengeneza nyuzi au madawa ya kulevya (bangi), n.k.
Spishi
- Cannabis indica Mbangi-dawa: hutoa bangi.
- Cannabis ruderalis Mbangi-wanja: hutumika kwa kuchavusha.
- Cannabis sativa Mbangi-katani: hutoa nyuzinyuzi hasa.
Matumizi ya Mbangi
Spishi hizo za mbangi zina matumizi mengi ya matibabu, ujenzi, kutengenezea dizeli oganiki na pia hufumwa nyuzi zinazotumika katika ushonaji. Utafiti kuhusu mbangi unaendelea kufumbua matumizi mengine zaidi. Shida yake kubwa ni kusababisha uraibu.[1][2][3][4]
Kinaganaga:
- Majani ya mmea wa kike wa Mbangi hutumika kutengeneza bangi. Bangi hutumika katika dawa ya kulevya kwa sababu inasababisha namna ya ulevi.
- Mbangi ni mmea wa nyuzinyuzi ambazo hufumwa nyuzi zinazotumika katika ushonaji wa vitu tofautitofauti.
- Mbangi, hasa spishi ya Cannabis sativa, hupasuliwa mbao, fito na vikingi za ujenzi.
- Kimatibabu sehemu tofauti za Mbangi hutumika kwa shughuli tofauti za tiba. Mbegu za Hemp hutumika kupunguza ugonjwa wa moyo kwa vile hutoa nitriki oksidi inayopumzisha mishipa ya damu na kushusha shinikizo la damu. Mafuta yatokayo kwa mbegu hizi za mbangi hutumika kutibu magonjwa ya ngozi. Mbegu za Mbangi Hemp pia zina asidi aina ya GLA (Gamma-Linolenic Acid) inayotumika kupunguza athari za prolactini inayosababisha dalili za kabla ya hedhi (Premenstrual Syndrome) wakati wa kukatika uzazi (menopause). Magonjwa mengine ambayo Mbangi una uwezo wa kutibu ni kama vile pumu, ugonjwa wa Parkinson, umbugiaji wa pombe kupindukia, woga wa kula (anoreksia nevosa), unyogovu, ugonjwa wa maungio ya mifupa (athritisi), gliomas, kifafa, shida ya kupumua usingizini (apnea) na glaukoma. Mafuta ya CBD inayotolewa kutoka kwa mbangi yanauwezo wa kutibu wasi wasi (anxiety) na huzuni (depression).
- Mbegu za mbangi pia zaweza kutolewa mafuta au dizeli oganiki inayoweza kutumika kwa jenereta au kuendesha injini nyingine za dizeli.[5]
- Utafiti unaendelea kuhusu uwezekano wa kutumia mbangi katika utengenezaji wa karatasi za kuandikia na kuhusu madhara yake kwa afya[6].
Picha
-
Majani
-
Maua dume
-
Maua jike
Tanbihi
- ↑ Reynolds, Peter (Februali 27, 2017). "Medicinal Cannabis: The Evidence" (PDF). CLEAR Cannabis Law Reform (kwa American English). Iliwekwa mnamo Agosti 6, 2018 – kutoka The BMJ Publishing Group Ltd.
{{cite journal}}
: Check date values in:|date=
(help) - ↑ International Association for Cannabinoid Medicine. "Clinical Studies and Case Reports". Cannabinoid Medicine - International Association for Cannabinoid Medicine Website (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-28. Iliwekwa mnamo 2018-08-06.
- ↑ ProCon.org. "60 Peer-Reviewed Studies on Medical Marijuana - Medical Marijuana - ProCon.org". ProCon.org Website (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-08-03. Iliwekwa mnamo 2018-08-06.
- ↑ Armentano, Paul; Carter, Greg; Sulak, Dustin; Goldstein, Estelle Toby (2018). "Emerging Clinical Application for Cannabis and Cannabinoids A Review of the Recent Scientific Literature" (PDF). Working to Reform Marijuana Laws (kwa American English) (tol. la Expanded and Revised Eighth Edition). The National Organization for the Reform of Marijuana Laws. Iliwekwa mnamo 2018-08-06 – kutoka The National Organization for the Reform of Marijuana Laws.
{{cite journal}}
:|edition=
has extra text (help) - ↑ "COOLFUEL Episode: Sugarcane and Hempoline". Iliwekwa mnamo 2009-10-16.
- ↑ In many communities, cannabis is perceived as a low-risk drug, leading to political lobbying to decriminalise its use. Acute and chronic cannabis use has been shown to be harmful to several aspects of psychological and physical health, such as mood states, psychiatric outcomes, neurocognition, driving and general health. Furthermore, cannabis is highly addictive, and the adverse effects of withdrawal can lead to regular use. These in turn have adverse implications for public safety and health expenditure. Although the cannabinoid cannabidiol (CBD) has been shown to have positive health outcomes with its antioxidant, anticonvulsant, anti-inflammatory and neuroprotective properties, high-potency cannabis is particularly damaging due to its high tetrahydrocannabinol (THC), low CDB concentration. It is this high-potency substance that is readily available recreationally. While pharmaceutical initiatives continue to investigate the medical benefits of CDB, “medicinal cannabis” still contains damaging levels of THC. Altogether, we argue there is insufficient evidence to support the safety of cannabis and its subsequent legalisation for recreational use. Furthermore, its use for medicinal purposes should be done with care. We argue that the public conversation for the legalisation of cannabis must include scientific evidence for its adverse effects. . http://www.eurekaselect.com/154161/article
Marejeo
Viungo vya nje
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mbangi kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |