Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Ufaransa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mfaransa)
République française Jamhuri ya Kifaransa
Bendera ya Ufaransa Nembo la Ufaransa
Bendera ya Ufaransa Nembo la Ufaransa
National motto: Uhuru, Usawa, Undugu
(Kifaransa: Liberté, Egalité, Fraternité)
Mahali pa Ufaransa
Lugha rasmi Kifaransa1
Mji mkuu Paris
Mji mkubwa Paris
Rais: Emmanuel Macron
Waziri Mkuu: Michel Barnier
Eneo
 - Jumla2


 - Ufaransa bara3



 - % maji
Nafasi ya 42
674,843 km²
(260,558 sq. mi.)
Nafasi ya 47
551,695 km²4
(213,011 sq. mi.)
543,965 km²5
(210,026 sq. mi.)
0.26%
Wakazi
(1 Januari 2023)
 - Total2
 - Ufaransa bara3
 - Density3
Nafasi ya 20

68,042,591
65,834,837
116/km²
GDP (PPP)
  - Jumla (2003)
  - GDP/mtu
Nafasi ya 5
$1.661 Trillioni
$27,600
Pesa Euro (€)6, CFP Franc7
Kanda ya wakati
 - in summer
CET (UTC+1)3
CEST (UTC+2)3
Wimbo wa taifa La Marseillaise
Internet TLD .fr
Calling Code 33

1 Taz. #Demografia kwa lugha za kimkoa
2 Eneo lote la Ufaransa pamoja na mikoa ya ng'ambo lakini bila Antaktika.
3 Ufaransa bara pekee (=Ufaransa ya Ulaya)
4 Namba za taasisi ya jiografia ya Ufaransa
5 Kumbukumbu ya ofosi ya ardhi
6 Jamhuri yote ya Kifaransa bila maeneo katika Pasifiki
7 Maeneo ya ng'ambo katika Pasifiki pekee

Ramani ya Ufaransa katika Ulaya.

Ufaransa ni nchi ya Ulaya na mwanachama mwanzilishi wa Umoja wa Ulaya.

Mji mkuu ni Paris.

Eneo lake ni km² 674,843; na idadi ya wakazi ni 63,044,000.

Imepakana na Ubelgiji, Luxemburg, Ujerumani, Uswisi, Italia, Monako, Andorra na Hispania.

Ufaransa ulikuwa kati ya nchi zenye makoloni mengi ikasambaza lugha yake kote duniani na kutunza uhusiano wa pekee na nchi nyingine zinazotumia Kifaransa.

Jiografia

Mnara wa Eiffel

Ufaransa ina pwani ndefu kwenye bahari ya Atlantiki pande za kaskazini na magharibi halafu kwenye Mediteranea upande wa kusini.

Ufaransa ina pia maeneo mengi ya ng'ambo yaliyokuwa makoloni yake zamani lakini kwa sasa ni sehemu rasmi za Jamhuri ya Ufaransa na wakazi wao ni raia wenye haki zote. Kati ya maeneo haya kuna hasa visiwa katika Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kusini, Bahari ya Karibi, Afrika, Bahari Hindi halafu Bahari ya Pasifiki.

Mito

Baadhi ya mito ya Ufaransa ni:

Historia

Historia ya awali

Ufaransa ulikaliwa na watu tangu muda mrefu sana. Utafiti wa akiolojia umeonyesha vifaa vya mawe vyenye umri wa miaka laki iliyopita.

Gallia

Watu wa Ufaransa waliingia katika historia andishi kupitia taarifa za waandishi wa Roma ya Kale walioeleza habari za majirani wao Wagallia katika Italia ya kaskazini na Ufaransa wa leo. Hao Wagallia walikuwa Wakelti na mara kwa mara katika hali ya vita kati yao na Waroma.

Kuanzia mwaka 58 KK Juliasi Caesar aliteka na kutawala Gallia yote kwa niaba ya Jamhuri ya Roma.

Gallia ikaendelea kuwa moja ya majimbo tajiri ya Roma na wakazi wengi walitumia lahaja za Kilatini kilichopata kuwa mama wa Kifaransa cha sasa. Lahaja za Kikelti zilibaki katika maeneo ya kando tu, kwa mfano Bretagne.

Polepole wakazi wengi walipata kuwa Wakristo wa Kanisa Katoliki.

Sehemu ya Milki ya Wafaranki

Wakati wa kuporomoka kwa Dola la Roma makabila ya Kigermanik waliingia katika eneo la Ufaransa na kuchukua utawala mikononi mwao.

Kabila la Kigermanik la Wafaranki[1] lilitawala sehemu kubwa ya Ufaransa pamoja na Ujerumani ya magharibi mnamo mwaka 500.

Mfalme wao Chlodvig I (tamka klod-vig) alipokea Ukristo wa Kikatoliki kama dini rasmi ya milki yake.

Mfalme Karolo Mkuu alipanua mipaka ya milki hadi Ujerumani ya kaskazini na Italia na mwaka 800 akapokea cheo cha Kaisari wa Roma kwa mikono ya Papa Leo III.

Chanzo cha ufalme wa Ufaransa

Baada ya kifo cha Karolo na mwanawe, milki iligawiwa kati ya warithi kwenye mkataba wa Verdun mwaka 843.

Miaka 100 baadaye mtemi wa Paris Hugo Capet alichukua nafasi ya wajukuu wa Karolo na wafuasi wake waliendelea kuimarisha mamlaka ya kifalme.

Ugawaji wa mwaka 843 ulikuwa chanzo cha Ufaransa kama nchi ya pekee. Mwanzoni ilijulikana kama "milki ya Wafaranki wa magharibi" ilhali sehemu za Ujerumani ziliitwa "milki ya Wafaranki wa mashariki". Lakini Wagermanik katika Ufaransa walikuwa wameshaacha lugha yao asilia na kutumia kile Kilatini-Kifaransa cha siku zile.

Wafalme wa sehemu walikuwa dhaifu mwanzoni na mamlaka kubwa ilikuwa mikononi wa makabaila katika majimbo ya ufalme.

Ufaransa na Uingereza

Kwa karne kadhaa historia ya Ufaransa ilikuwa na ugumu wa pekee kutokana na mchanganyiko wake na historia ya Uingereza. Mwaka 1066 mtemi William wa Normandi aliyekuwa chini ya mfalme wa Ufaransa alivamia Uingereza na kuwa mfalme huko lakini yeye pamoja na warithi wake waliendelea kuwa watemi wa jimbo la Normandi. Kwa njia hiyo watemi wa Normandi waliingia mara nyingi kwa nguvu katika siasa ya Ufaransa.

Baada ya kifo cha mtawala wa mwisho kutoka ukoo wa Hugo Capet Wanormandi walidai cheo cha mfalme wa Ufaransa na hii ilikuwa chanzo cha vita ya miaka 100. Mwishowe Waingereza walipaswa kuacha karibu mali yote kutoka urithi wa Wanormandi.

Kilele cha ufalme hadi mapinduzi ya 1789

Francia, 1703

Milki ya Ufaransa iliendelea kuwa nchi yenye nguvu katika Ulaya.

Katika vita ya miaka 30 (1618 - 1648) iliweza kujipatia nafasi ya mwamuzi katika siasa ya Ulaya bara.

Wakati huohuo matengenezo ya Kiprotestanti yalikuwa yameshaenea na watemi Waprotestanti walitawala maeneo makubwa ya Ufaransa.

Mfalme Louis XIV wa Ufaransa aliona hali hiyo kama hatari kwa mamlaka yake, akafuta ahadi zote kwa Waprotestanti hadi wakaondoka nchini kwa wingi.

Baada ya Louis XIV, waandamizi wake waliongeza madeni ya serikali kwa vita vingi dhidi ya Uingereza na ujenzi wa majumba makubwa.

Matatizo makali ya kiuchumi pamoja na mawazo mapya ya Zama za Mwangaza yalisababisha mapinduzi ya Kifaransa ya mwaka 1789.

Mamlaka ya mfalme iliondolewa na baada ya kipindi jamhuri kutangaziwa ilhali mfalme alishtakiwa kuwa msaliti na kupewa adhabu ya mauti.

Napoleone

Baada ya mapinduzi, Ufaransa uliingia katika vita na falme nyingine za Ulaya zilizoona mapinduzi ni hatari kwao. Wapinzani walikuwa hasa Uingereza, Austria na pia Prussia. Kwa jumla jeshi la kimapinduzi lilifaulu kutetea eneo la Ufaransa na kuingia katika sehemu za Ujerumani, Uholanzi na Italia.

Katika vita hivyo afisa kijana, kwa jina Napoleon Bonaparte, alipanda vyeo haraka hadi kuingia katika siasa; mwaka 1799 alichukua mamlaka yote kwa kutumia cheo cha "konsuli wa kwanza" na tangu 1804 alijiita "Kaisari wa Wafaransa".

Katika vita vya mfululizo aliteka sehemu kubwa ya nchi za Ulaya au kuzilazimisha kumfuata. Baada ya kushinda Prussia na Austria na kutawala Italia pamoja na Hispania alikuwa mkuu wa Ulaya.

Lakini vita alivyoanzishwa mwaka 1812 dhidi ya Urusi vilikuwa msingi wa kushindwa kwake.

Mwaka 1814 alipaswa kusalimu amri, akapelekwa kwenye kisiwa cha Elba (Italia); aliporudi barani na kujaribu kuwa mkuu wa Ufaransa tena, jeshi lake lilishindwa katika mapigano ya Waterloo mwaka 1815 na Napoleon akawa mfungwa kwenye kisiwa cha St Helena hadi kifo chake.

Karne mbili za mwisho

Baadaye ufalme ulirudishwa kwa msaada wa nchi zilizoshauriana pamoja kwenye mkutano wa Vienna 1815, lakini ulipinduliwa tena.

Katika karne ya 19 Ufaransa ulijitwalia makoloni mengi, hasa Afrika.

Katika vita vikuu vya kwanza, ulivamiwa na Wajerumani, lakini mwisho uliibuka na ushindi na kurudishiwa mikoa ya Alsace na Lorraine iliyotekwa na Ujerumani katika vita vya mwaka 1870.

Baada ya vita vikuu vya pili ambako nchi ilitekwa na Ujerumani kwa kiasi kikubwa, Ufaransa ulipata katiba mpya na kujiunga na NATO (1949) na mwanzo wa Umoja wa Ulaya (tangu 1951). Ilihesabiwa kati ya washindi wa vita na kupata kiti cha kudumu kwenye Baraza la Usalama la UM.

Wakati huohuo utawala wake juu ya makoloni ulianza kuporomoka. Baada ya kushindwa katika Vita vya kwanza vya Indochina mwaka 1954 Ufaransa ulipaswa kukubali uhuru wa Vietnam Kaskazini, Vietnam Kusini, Laos na Kambodia.

Makoloni yake mengi katika Afrika yalipata uhuru bila vita mnamo 1960. Ila Aljeria, iliyowahi kutangazwa kuwa sehemu ya Ufaranya yenyewe, ilipata uhuru wake baada ya vita vikali vya kupigania uhuru vya miaka 1954 - 1962.

Katika kipindi hiki cha vurugu jenerali Charles de Gaulle alichaguliwa kuwa rais chini ya katiba mpya iliyounda mfumo wa rais kama kiongozi wa serikali mwenye mamlaka makubwa.

Vyama mbalimbali vilivyoendelea kutetea itikadi ya de Gaulle hata baada ya kifo chake vinaendelea kuwa mkondo muhimu katika siasa ya Ufaransa na marais walichaguliwa ama kutoka mkondo huo (Jaques Chirac, Nicolas Sarkozy) au kutoka Chama cha Kisoshalisti (Francois Mitterand, Francois Hollande).

Tangu miaka ya 1980 chama kipya cha Front National kilianza kupata kura kikipinga uhusiano wa karibu na Umoja wa Ulaya na wahamiaji Waislamu kutoka nchi za Afrika ya Kaskazini.

Katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2017 ilitokea kwa mara ya kwanza ya kwamba wagombea wa vyama vikubwa walishindwa kupata kura nyingi na awamu ya mwisho ya uchaguzi ilikuwa kati ya mgombea wa kujitegemea Emmanuel Macron (aliyepata urais) na Marine Le Pen wa Front National.

Utawala

Baada ya mapinduzi ya mwaka 1789 Ufaransa yote iligawiwa katika wilaya (kwa Kifaransa "département") zilizoongozwa na mkuu (prefect) aliyekuwa mwakilishi wa serikali kuu.

Tangu mwaka 1964 wilaya ziliwekwa chini ya ngazi mpya ya mikoa ("région").

Tangu mwaka 1982 Ufaransa ilianza kutumia mfumo wa ugatuzi na kuipa mikoa, wilaya na kata zake kiwango cha madaraka ya kujitawala. Mikoa huwa sasa na bunge zao.

Kiasili Ufaransa ya Ulaya ilikuwa na mikoa 22. Idadi hiyo ilipunguzwa mwaka 2016. Kwa sasa kuna mikoa 13 Ufaransa ya Ulaya halafu mikoa 5 ya ng'ambo huko Amerika Kusini na katika Bahari Hindi.

Majiji

  1. Paris
  2. Lyon
  3. Marseille
  4. Toulouse
  5. Toulon
  6. Lille
  7. Brest
  8. Nice
  9. Amiens
  10. Angers
  11. Bordeaux
  12. Caen
  13. Dijon
  14. Metz
  15. Nantes
  16. Nîmes
  17. Rennes
  18. Montpellier
  19. Grenoble
  20. Strasbourg
  21. Saint-Étienne

Watu

Toka muda mrefu Ufaransa imepokea wahamiaji wengi, hivi kwamba 7.7% za wakazi ni wageni; tena 23% wana walau mzazi au babu/bibi mmoja aliyezaliwa nje ya nchi. 13% za wakazi wana asili ya Afrika (kaskazini au kusini kwa Sahara).

Lugha ya taifa ni Kifaransa lakini kuna lugha za maeneo kama vile Kibaski, Kibretoni, Kikatalani, Kikorsika, Kijerumani, Kiholanzi na Kioksitania. Wahamiaji kutoka nchi zilizokuwa makoloni ya Ufaransa walileta pia lugha zao, hasa Kiarabu na Kiberber kutoka Afrika ya Kaskazini.

Ufaransa haina dini rasmi lakini wakazi walio wengi (47%) ni Wakatoliki. 2% ni Waprotestanti na 1% Wakristo wengine. 4% ni Waislamu kutokana na wahamiaji milioni 5-6 kutoka makoloni ya zamani katika Afrika ya Kaskazini au Magharibi pamoja na watoto wao. 2% ni Wabuddha na 1% Wayahudi. 33% hawana dini yoyote[2].

Wafaransa wanapenda sana michezo, hasa mpira wa miguu.

Watu maarufu

Tazama pia

Tanbihi

  1. jina la Kilatini "Franci" ni asili ya maneno kama "Ufaransa, Kifaransa" na pia "Frankonia" inayotaja sehemu ya Ujerumani - hasa Bavaria kaskazini- ambako watu hujiita "Franken" hadi leo. Maumbo tofauti kwa Kiswahili yametokea na jina asilia; yaani herufi "c" ilipata mara matamshi kama "k" (Franki) au "s" (-faransa)
  2. "Etat des lieux de la laïcité en France - 2021" (PDF) (official statistics) (in French). Observatoire de la laïcité, Government of France.

Viungo vya nje


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ufaransa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.