Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Mkoa wa Pwani (Kenya)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa mkoa wa Pwani katika Kenya

Mkoa wa Pwani ni kati ya mikoa nane ya Kenya ukipakana na Bahari Hindi, Tanzania na mikoa ya Kenya ya Bonde la Ufa , Mashariki na Kaskazini-Mashariki.

Makao makuu ya mkoa yapo Mombasa.

Mkoani kuna wilaya zifuatazo (makao makuu katika mabano):

Mombasa ndipo ilipo bandari kuu ya Kenya. Kuna maeneo muhimu ya utalii kama Malindi na sehemu za pwani kusini (Diani)na kaskazini (Kikambala) ya Mombasa. Eneo la Voi katika mkoa wa Pwani ni maarufu kwa kulima makonge.

Historia ya Mkoa wa Pwani

[hariri | hariri chanzo]

Pwani la Kenya ni nchi ya miji ya Waswahili hasa. Miji hii kama vile Lamu, Mombasa, Malindi, na mengine mengi iliyokuwa vituo vya biashara ya kimataifa tangu zaidi ya miaka 1000 iliyopita. Upepo wa monsuni ulibeba jahazi kutoka Uarabuni, Uajemi hata Bara Hindi kwenda pwani la Afrika ya Mashariki. Monsuni ulipogeuka kila baada ya nusu mwaka jahazi ziliweza kurudi kwao na bidhaa za biashara. Hivyo vituo vya biashara na mapumziko vikawa miji ya Waswahili, utamaduni uliounganisha tamaduni za wafanyabiashara Waarabu au Waajemi na Waafrika wenyeji wa pwani.

Miji ya kwanza ya Waswahili ilikuwa Lamu na Pate. Wakati wa kuja kwa Wareno mnamo mwaka 1500 BK Malindi na Mombasa ilikuwa miji muhimu zaidi.

Pwani ina pia magofu ya miji kama Gedi iliyokwisha bila sababu zake kueleweka.

Pwani limekuwa sehemu ya Usultani wa Zanzibar wakati wa karne ya 19 BK. Baada ya kuja kwa ukoloni wa Uingereza mwisho wa karne hiyo ya 19. BK Sultani wa Zanzibar alikodisha pwani kwa Wakoloni. Mwaka 1964 pwani lilikuwa sehemu ya nchi mpya ya Kenya.