Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Msaada:Maana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Makala ya maana ina kazi ya kumwelekeza msomaji mahali anapotafuta kama neno moja lina maana mbalimbali. Mara nyingi neno lina maana mbalimbali. Jina maalum inaweza kutaja watu na mahali mbalimbali. Lakini kila makala ya wikipedia inapaswa kuwa na jina tofauti. Kwa sababu hiyo tunapaswa kutafuta majina tofauti kwa makala zinazohusu maana tofauti ya jina lilelile.

Mfano wa makala ya maana kuhusu "Mwezi"

Makala ya maana inakusanya maana hizi zote kwenye ukurasa wa pamoja. Haina maandishi marefu bali maelezo mafupi tu mfano: .

  1. mwezi (gimba la angani) - msindikizaji wa sayari
  2. mwezi (wakati) - mojawapo wa vipindi kumi na mbili vya mwaka

Vivyo hivyo:

  1. Ndege (mnyama) - aina wa wanyama ambao kwa kawaida wanaweza kuruka
  2. Ndege (uanahewa) - chombo cha usafiri kinachoweza kuruka wakati kikiwa na abiria au mizigo ndani yake

Isipokuwa kama maana mbalimbali yana historia ya pamoja au uhusiano wa pekee ni sawa kuongeza chini ya orodha ya viungo maelezo ya ziada. Zisihusu viungo moja-moja. Mfano:

Majengo inataja mahali pengi Afrika ya Mashariki kwa hiyo tunatofautisha Majengo (Kigoma), Majengo (Mbeya mjini) na kadhalika. Mitaa au kata hizi zote zina historia ya kufanana inayoelezwa chini ya orodha.

Makala ya maana inapaswa kuwa na {{Kigezo:Maana}} chini yake.

Tahadhari ya kutafsiri makala za maana kutoka lugha nyingine

[hariri | hariri chanzo]

Hakuna ubaya kutafsiri makala za maana, kwa mfano kutoka wikipedia ya Kiingereza (disambiguation page). Inaweza kusaidia kwa mfano tukiangalia majina ya kijiografia (visiwa, miji, mito) yanayopatikana mara nyingi duniani. Lakini lazima kutumia akili kwa sababu uwingi wa maana katika lugha moja hautafsiriki kwa lugha nyingine moja kwa moja. Hasa kama ukurasa wa "disambiguation" inajumlisha pia neno husika kama jina maalumu ni marufuku kutafsiri majina yale. Linganisha: Wikipedia:Makosa#7 Kutafsiri majina maalumu.