Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Umba (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mto Umba)
Ramani ya mto Umba.

Umba ni mto wa Tanzania kaskazini mashariki unaopita katika Mkoa wa Tanga na kuishia nchini Kenya.

Chanzo chake kipo katika milima ya Usambara katika msitu wa Shagayu kwa kimo cha mita 2,000 juu ya UB.

Unapita Mlalo na kuendelea kutelemka haraka kuelekea pwani ikipokea mito ya kando kutoka milima ya Usambara[1].

Kilomita chache kabla ya kufika Bahari ya Hindi inavuka mpaka wa Kenya (kaunti ya Kwale).

Mdomo wa Umba kwenye bahari hiyo ulipangwa mwaka 1890 baina ya Ujerumani na Uingereza kuwa mpaka wao. Hadi leo sehemu hii ni chanzo cha mstari wa mpaka kati ya Tanzania na Kenya unaoendelea bila kunyoka hadi Ziwa Jipe, ukifuata mitelemko ya mlima Kilimanjaro na kuendelea hadi Ziwa Viktoria.

Tangu miaka ya 1960 vito mbalimbali vimepatikana katika maeneo ya juu ya Umba.[2] Kuna hifadhi ya wanyamapori ya mto Umba, pamoja na hifadhi ya Mkomazi, jumla kilomita za mraba 2,600.

Beseni la mto Umba huwa na km² 8,070 na kati ya hizo km² 2,560 ziko upande wa Kenya. Matawimto mengi yanaingia kutoka kusini, chache kutoka kaskazini. Beseni la Umba hupokea takriban milimita 600 za mvua kwa mwaka.[3]

Hidrometria

[hariri | hariri chanzo]

Kiasi cha maji kinachopita katika Umba kimepimwa kwenye kituo cha Mbuta takriban km 40 kabla ya mdomo wake. Hapo chini ni wastani ya kiasi cha maji kwa /s kwenye kituo cha Mbuta kwa kipindi cha miaka 30 ya 19541984)[4]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. suchname:umba Ilihifadhiwa 17 Mei 2017 kwenye Wayback Machine., makala Umba katika Kamusi ya Koloni za Kijerumani
  2. [https://www.mindat.org/loc-8265.html Umba River (Umba Valley), Tanga Region, Tanzania] kwenye tovuti ya mindat.org, iliangaliwa Februari 2017
  3. https://portals.iucn.org/library/efiles/documents/2009-073.pdf IUCN Eastern and Southern Africa Programme, 2009. The Pangani River Basin: A Situation Analysis, 2nd Edition, uk. 74
  4. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-09-07. Iliwekwa mnamo 2017-02-03.
  • Fred Simon Lerise: Facilitating Cross-Border Dialogue, The Case of Umba River Ecosystem in Kenya and Tanzania, Uni Siegen Summer School 2005

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Umba (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.