Location via proxy:   [ UP ]  
[Report a bug]   [Manage cookies]                
Nenda kwa yaliyomo

Muhammadu Buhari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Buhari

Muhammadu Buhari (amezaliwa tar. 17 Desemba 1942) amekuwa rais wa Nigeria tangu 29 Mei 2015. Anashika cheo mara ya pili maana aliwahi kuwa rais toka 31 Desemba mwaka 1983 hadi 27 Agosti mwaka 1985. Wakati ule aliingia madarakani kama jenerali ya jeshi kwa kumpindua rais aliyechaguliwa Shehu Shagari. Buhari mwenyewe alipinduliwa mwaka 1985 na jenerali Ibrahim Babangida.

Katika kura za uchaguzi za miaka 2003, 2007 na 2011 aligombea urais bila kufaulu. alikuwa mgombea urais katika uchaguzi wa kitaifa wa mwaka huo, lakini hakuibuka kuwa mshindi. Alirudia kugombea katika kura ya mwaka 2015 aliposhinda dhidi ya rais Goodluck Jonathan kwa asilimia 54 za kura zote.[1]

Muhammadu Buhari katika awamu la kwanza la urais alitanguliwa na Shehu Shagari kisha akafuatiwa na Ibrahim Babangida.

  1. Muhammadu Buhari sweeps to victory (Guardian UK 31 Machi 2015)

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Muhammadu Buhari kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.