Nasaba ya Han
Mandhari
Nasaba ya Han (kwa Kichina cha asili: 漢朝 ; Kichina rahisi: 汉朝; Hanyu Pinyin: Hàn cháo; Wade-Giles: Han Ch'au; 206 KK – 220 BK) ilitawala Uchina baada ya nasaba ya Qin, na ilitangulia Madola Matatu. Utawala huu ulianzishwa na familia maarufu iliyofahamika kama ukoo wa Liu.
Watu wa China huhesabu nasaba ya Han iliyodumu kwa karne nne kuwa kati ya vipindi vikuu katika historia yote ya nchi. Hivyo, jamii kubwa ya China hujihesabu mpaka leo “watu wa Han”, kwa heshima ya familia ya Han na utawala waliouanzisha.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nasaba ya Han kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |